Skip to main content

Newsletter block in header

prev
next

You are here

Kuhusu MSF

Msaada wa Matibabu ambako unahitajika zaidi

 

Timu ya wafanyakazi wa MSF inafanya kazi katika nchi zaidi ya 65 duniani kwa kutoa msaada wa kuokoa maisha kwenye maeneo ambayo unahitajika zaidi. Wafanyakazi 30,000 wanahudumu katika maeneo yenye migogoro, milipuko ya magonjwa, majanga ya asili na maeneo ambayo watu hawana uwezo wa kupata huduma za matibabu. Tunafanya kazi kwa misingi ya uhuru, kutofungamana na upande wowote na kwa uadilifu; Tunatoa msaada kwa watu ambao wanauhitaji zaidi bila kujali ni akina nani, wanatoka wapi, msimamo wao kisiasa au imani ya dini.

Shirika sasa lina miradi mikubwa ya matibabu katika ukanda wa nchi za Afrika Mashariki ikiwemo Sudan, Sudan Kusini, Kenya, Tanzania, Uganda, Ethiopia, Somalia na Burundi. Katika nchi hizi, MSF inasimamia hospitali, vituo vya afya na Kliniki zinazotembea na kuanzisha huduma za miradi ya dharula kadiri mahitaji yanavyojitokeza.

MSF ina ofisi ya kanda nchini Kenya  ambayo inasaidia miradi ya kutoa matibabu nchini humo yo na nchi zinazoizunguka, inaajiri wafanyakazi kusaidia operesheni zake duniani pamoja na kueneza uelewa kuhusu majanga ya kibinadamu ambayo tumekuwa tukikabiliana nayo. MSF ina kitengo maalumu cha ubunifu (Kinachofahamika kama “kitengo cha kuhudumia watuwanaokimbia’, kitengiambacho kinasaidia miradi yake duniani kote pamoja na kuwa na kituo cha usambazaji nchini Kenya.