Skip to main content

Newsletter block in header

prev
next

You are here

Shirikisho la MSF


MSF ni vuguvugu linaloundwa na watu kutoka kona zote za dunia na ambao wana lengo moja ambalo ni kuokoa maisha na kupunguza mateso ya watu kwa kutoa huduma za afya ambako zinahitajika zaidi.

 Mafanikio yetu katika kipindi cha miaka 40 ni ushuhuda kwa watu hawa ambao wamejitolea muda na utaalamu wao kwa MSF na kufanya kazi ndani na nje. 

Kuendeleza mafanikio haya ya wafanyakazi wetu, yaliyopita na ya sasa kunaweza kunajenga mustakabali wetu na kuwa mjumbe wa shirikisho la MSF. 

Kila ofisi 23 za MSF ni shirikisho - shirika linamilikiwa na wajumbe ambao sio tu wanatengeneza muundo na kulinda kazi za ofisi za MSF, lakini pia wanaungana kutengeneza mustakabali mzuri wa vuguvugu la MSF.

Kuwa mwanachama kunamaanisha kuwa unawajibika kwa pamoja kwaajili ya MSF. Na kwasababu watu wanaofanya maamuzi wamefanya kazi na MSF, shirika linabaki kujikita katika utoaji huduma za matibabu na kubakia na msingi wetu wa Kuwa huru, kutofungamana na upande wowote na uadilifu. Pia kunaifanya MSF kuwa vuguvugu la kidunia, tumejikita kutoa msaada wa matibabu duniani na hasa katika maeneo yenye changamoto.

 

Shirikisho la MSF la Afrika Mashariki


Shirikisho la Afrika Mashariki la MSF (EAA) linaundwa na wajumbe wa sasa na wale wa zamani waliofanya kazi na MSF, na linahusisha nchi 7 za Afrika Mashariki ikiwemo Burundi, Eritrea, Ethiopia, Kenya, Rwanda, Sudan, Somalia, Sudan Kusini, Djibouti, Tanzania na Uganda.

Wajumbe wa shirikisho wanachagua wajumbe wa bodi, ambao wanaongoza shirikisho kwa niaba yao. Wajumbe wa bodi wanakutana mara tatu kwa mwaka, wanafanya mikutano ya kwenye mtandao mara 6 kwa mwaka, wakijadiliana kuhusu masuala ya MSF kwenye ukanda na duniani.

Shirikisho hili pia linafanya mkutano mkuu wa mwaka katika moja ya nchi mwanachama kila mwaka, ambapo wajumbe wa shirikisho wanaalikwa kuhudhuria na kusaidia kutoa uelekeo wa shirikisho katika miaka ijayo. Wajumbe pia wanashiriki katika majadiliano na mazungumzo kusaidia kujenga mustakabali wa MSF

Uanachama wa shirikisho uko wazi kwa wajumbe wa sasa na wale wa zamani waliofanya kazi na MSF kutoka duniani kote. Ikiwa unavutiwa kujiunga na shirikisho la MSF la Afrika Mashariki, tafadhali tuma barua pepe kwenda: [email protected]

 

Vuguvugu la MSF

Kila mwaka, wawakilishi waliochaguliwa  kutoka Afrika Mashariki wanakutana na wenzao kutoka mashirikisho ya MSF, wanachangia sauti zo katika mjadala wa kidunia ili kuzijenga kazi za MSF.

 Wakati wa mkutano wa kimataifa wa mwaka ambao ni wajuu kiutendaji katika MSF na ambapo wanachama wa mashirikisho wanakutana, rais wa MSF anachaguliwa na wawakilishi wa IGA. Bodi ya kimataifa pia inachaguliwa wakati wa mkutano mkuu. Wanawajibika kwa kuleta uwiano kwaajili ya hamasa yetu na vuguvugu lenye mabadiliko.

 

Nani anaweza kuwa mjumbe wa shirikisho?

Wafanyakazi walioko kwenye maeneo ya kazi, wale walioko ofisini na wale wa kujitolea wanaweza kuomba kujiunga baada ya kufanya kazi na MSF kwa kipindi maalumu. Kwa mjumbe wa shirikisho la Afrika Mashariki mmoja anatakiwa kuwa amefanya kazi kwa miezi 6, miezi 12 kama mfanyakazi katika ngazi ya kitaifa au miaka miwili kwa kujitolea katika makao makuu. Mchango wao kwa MSF unaweza kuwa wa operesheni yoyote katika nchi yoyote.