Skip to main content

Newsletter block in header

prev
next

You are here

Wajibu wetu kwa mwenendo mzuri wa tabia

MSF inajiona kama muajiri muwajibikaji na mshirika, na hili linajikita katika mwenendo mzuri wa tabia kwa wanachama wake. 

Kuna makubaliano ya pande mbili na heshima kwa muajiriwa na muajiri ili kuzuia, kubaini na kuzungumzia tabia isiyokubalika na mfanyakazi wa MSF ni lazima atumie njia ya kuwafahamisha wagonjwa na unufaikaji wa moja kwa moja unaotokana na tabia zilizoanishwa hapa chini.

Ndani ya MSF, wale wote ambao ni sehemu ya wafanyakazi (waajiriwa, wakiwemo wafanyakazi walio katika majukumu ya kimataifa, wanaojitolea na wafanyakazi wa kila siku) na washirika (wakiwemo washauri na wageni) wanaelewa na kuheshimu matakwa yaliyoanishwa hapa chini, kuyatumia katika majukumu yao ya kikazi na binafsi na kuyatii.

Ikiwa hili halitakuwa tatizo, MSF inatoa nafasi ya kuripoti katika ngazi zote za shirika na jambo lolote lisiloshughulikiwa litakabiliwa na vikwazo.

Tabia hizi zinatazamwa kama tabia za kiwango cha kawaida, na kanuni zaidi zinaweza kutumiwa kwa wafanyakazi wa MSF kulingana na mazingira ambayo wanafanya kazi na maeneo ya shughuli zao.

Tabia hitajika

1. Mfanyakazi wa MSF na washirika wake watatakiwa kujiheshimu na kutowabagua wagonjwa, wafanyakazi wenzao au wafanyakazi wa eneo husika kutokana na rangi za ngozi yao, mtazamo, aina ya maisha, jinsia, jinsi, hali ya kiuchumi, asili, dini, au imani na aina nyingine zozote.

2. Mfanyakazi wa MSF na washirika wake hawatamdhalilisha yeyote, (kwa kumpiga, kingono au aina nyingine yeyote ya udhalilishaji) au kisaikolojia ( kumdharau, kutumia madaraka vibaya, kumbugudhi, kumbagua au upendeleo);

3. Mfanyakazi wa MSF na washirika wake hawatakubali kwa namna yeyote ile, tabia ambayo zinawanyanyasa watu wasionacho katika ukubwa wowote ule (mfano, kingono, kiuchumi au kijamii n.k). Inajumuisha ubadilishaji wa vitu, marupurupu au kutoa huduma kwa kutaka ngono, ikiwemo kuwatumia wanaojiuza kingono wakati ukiwa kwenye majukumu;

4. Mfanyakazi wa MSF na washirika wake hawatakubali vitendo vya udhalilishaji wa watoto, unyonyaji na ukatili na kutojihusisha kingono na watoto;

5. Mfanyakazi wa MSF na washirika wake hawatatumia vibaya nafasi zao kujinufaisha. Kila mfanyakazi atatumia rasilimali za MSF (ikiwemo maeneo, vitu, fedha, hadhi, wasifu n.k) kwa kuheshimu na kujali kwa maslahi ya shirika na watu ambao inategemea kuwahudumia.

Kuhamasisha mazingira mazuri ya kazi yaliyo huru bila bugudha, unyonyaji na udhalilishaji

Pata maelezo zaidi