Tunatumia asilimia 84 ya fedha tunazokusanya kuendesha miradi yetu, ni asilimia 2 tu ndio tunaitumia kwa shughuli za kiutawala na gharama za wafanyakazi. Zinazobakia tunaziwekeza katika kufanya harambee..
Zaidi ya asilimia 90 ya fedha tunazokusanya zinatoka kwa watu binafsi wanaotoa kidogo, wachangiaji binafsi ambao wanatuamini kutumia fedha zao kule zinakohitajika zaidi, uhuru huu wa matumizi ya fedha unaturuhusu sisi kufika kwa haraka katika maeneo yenye dharula. Fedha nyingine zote zinatoka kwa mashirika ya kimataifa, taasisi na Serikalini.
Wakati tunapofanya kazi kwenye maeneo ambayo kuna pande nyingi zinazohusika na mgogoro, tunaegemea zaidi michango ya watu binafsi ili kuwa huru na kutofungamana na upande wowote, hii inatusaidia kuhakikisha tunatoa msaada kwa watu ambao wanahitaji zaidi, huru kutokana na mitazamo ya kisiasa.
Tunawajibika kwa wafadhili wetu ka umakini mkubwa, na tuna uwazi kuhusu kuhusu namna tunavyotumia fedha ambazo wametuamini kutupa. Kila mwaka, tunachapisha taarifa ya fedha ya mwaka, ikieleza kwa kina fedha tulizotumia kwenye miradi yetu yote.