Skip to main content

Newsletter block in header

prev
next

You are here

Kuhamasisha mazingira mazuri ya kazi yaliyo huru bila bugudha, unyonyaji na udhalilishaji.

Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) linahamasisha mazingira ya kazi ambayo ni huru kutokana na bugudha na udhalilishaji. Uongozi wetu umejikita katika kuhakikisha unaweka miundombinu na hatua za kufuata ili kuzuia na kutolea suluhu masuala ya udhalilishaji na bugudha. Wafanyakazi wote wanatarajiwa kuheshimu  kanuni za MSF kuhusu tabia na misingi yake kama ilivyoainishwa kwenye mkataba wake.

Uadilifu wa shirika unashikiliwa na tabia ya kila mtu ambaye ni mfanyakazi katika eneo lolote, kwa kuheshimu jamii tunayoihudumia. Kwetu sisi, inamaanisha kutovumilia tabia zozote kutoka kwa wafanyakazi wetu ambazo zinawalaghai watu walio kwenye mazingira magumu au kwa wafanyakazi kutumia nafasi zao kujinufaisha.

Utaratibu wa Malalamiko
Utaratibu, ikiwemo utaratibu wa kuwasilisha malalamiko umewekwa kulinda, kubaini, kuripoti na kudhibiti tabia zisizofaa, bugudha na udhalilishaji. Kupitia taratibu hizi, wafanyakazi wote wanashauriwa kuripoti mienendo mibaya au udhalilishaji ama kwa kupitia ngazi za uongozi au kutumia njia nyingine ambazo ni nje ya ya utaratibu au ngazi za juu kwa kutumia barua pepe maalumu. Wahanga au mashuhuda kwenye jamii kama ilivyo kwa wafanyakazi wa MSF wanashauriwa kuripoti mienendo yoyote mibaya kwetu ili tuhuma ziweze kushughulikiwa ipasavyo.

Kampeni za kueneza uelewa zinafanyika ili kutoa taarifa kwa wafanyakazi kujua taratibu zilizopo ili waripoti vitendo vya udhalilishaji. Taarifa hii hutolewa kupitia njia maalumu za mawasiliano, ikiwemo waraka wa wafanyakazi na zinatolewa pia kupitia vikao, kutembelea maeneo ya kazi na kupitia mafunzo. Hata hivyo, taarifa za kimtandao na mitaala ya mafunzo kuhusu tabia na udhibiti wa vitendo vya udhalilishaji hutolewa mara kwa mara na zimeboreshwa.

Mwaka 2018 kumeshuhudiwa shughuli katika maeneo haya na kuongezwa kwa wafanyakazi katika timu inayoangazia tabia za wafanyakazi; kuendelezwa kwa mfumo mpya wa kueneza uelewa, kuzuia na kubaini tabia zisizokubalika; na pia maboresho ya ukusanyaji wa taarifa na kuzitawanya kwa majukwaa yote ya MSF. Ni muhimu kukubali kuwa kuongezeka kwa taarifa kutoka kwa uma kumechangia pakubwa kueneza uelewa na uripotiji wa tabia zisizokubalika.

Kushughulikia taarifa kwa usiri.
MSF inalenga kuhakikisha kuwa taarifa kama hizi zinashughulikiwa kwa usiri mkubwa, ili kutengeneza mazingirra ambayo watu watajisikia wako salama kutoa malalamiko yao bila kuogopa kuhusu usalama wao, kazi zao au usiri wao.

Jukumu letu la kwanza pale tabia zisizokubalika zinaripotiwa ni usalama na afya ya waathirika. Suala hushughulikiwa kwa haraka sana kwa kuwasaidia ikiwemo msaada wa kisaikolojia na kimatibabu na kuwapatia msaada wa kisheria.

MSF mara zote inaheshimu uamuzi wa waathirika ikiwa wanataka au hawataki kulipeleka suala lao kwenye mfumo wa kisheria. Katika tukio la udhalilishaji wa kingono dhidi ya watoto, sera ya MSF ni kuliripoti suala hilo kwa mamlaka za kisheria kutegemea maslahi ya mtoto na upatikanaji wa utaratibu husika.

Changamoto kuu: Kupunguza vikwazo katika kutoa taarifa
Wakati takwimu za mwaka 2018 zikionesha kuongezeka kwa utolewaji wa taarifa kwa tabia zisizokubalika ukilinganisha na mwaka 2017, bado tunaamini kuwa vitendo hivi vinapewa makadirio ya chini sana, na hii huenda inatokana na changamoto za kuripotiwa kwa kiwango cha chini na ukusanyaji wa taarifa zenyewe.

Katika mwaka 2018, MSF ilikuwa na wafanyakazi elfu 43 waliokuwa wanafanya kazi kwenye maeneo mbalimbali. Tumeona kuongezeka kwa idadi ya tahadhari na malalamiko yaliyorekodiwa mwaka 2018, ambapo jumla ya malalamiko 356 yaliwasilishwa, ikiwa ni ongezeko la kutoka malalamiko 182 mwaka 2017. Takwimu hizi zinahusiana na tahadhari na malalamiko yaliyotolewa kwenye maeneo tunakofanyia kazi, lakini hayahusishi ofisi za makao makuu yetu. Tuna imani kuwa takwimu hizi ni ishara kuwa ni kutokana na uhamasishaji tulioufanya kwa watu kujitokeza.

Katika malalamiko hayo, baada ya uchunguzi malalamiko 134 yalithibitishwa ama kuwa ni yale ya udhalilishaji au tabia zisizokubalika (malalamiko 83 mwaka 2017). Idadi hii inajumuisha kesi 78 ambazo zilikuwa za udhalilishaji ukilinganisha na kesi 61 za udhalilishaji mwaka 2017. (Matukio haya yanajumuisha aina nyingi za udhalilishaji ikiwemo udhalilishaji wa kingono, bugudha na unyonyaji, matumizi mabaya ya madaraka, bugudha za kisaikolojia, ubaguzi na vitendo vya kudhuru mwili). Jumla ya wafanyakazi 52 walifutwa kazi kutokana na aina zote hizi za udhalilishaji katika mwaka wa 2018 (kulikuwa na wafanyakazi 58 waliofutwa kazi mwaka 2017).

Katika vitendo vya udhalilishaji 78, kesi 59 zilikuwa ni za udhalilishaji wa kingono, bugudha na unyonyaji, ikiwa ni ongezeko la kutoka kesi 32 mwaka 2017. Wafanyakazi 36 waliondolewa kazini kutokana na kesi hizo katika mwaka 2018 ikiwa ni ongezeko la kutoka kesi 20 katika mwaka 2017. 

Kulikuwa na kesi 56 zilizothibitishwa kuwa ni tabia zisizokubalika, ikiwa ni ongezeko la kutoka kesi 22 katika mwaka 2017 (tabia zisizokubalika zinajumuisha, kutowahudumia watu vizuri, kuwa na mahusiano nao, tabia zisizokubalika ambazo zinaenda kinyume na morali ya timu, na matumizi ya vilevi).

Tunaendelea kutoa wito kwa wafanyakazi, wagonjwa na mwingine yeyote ambaye atakutana na MSF kutoa taarifa ya matukio ambayo ni ya tabia zisizokubalika ambazo wamekumbana nazo.

Sababu za matukio haya kutoripotiwa kwa kiwango kikubwa ni pengine kutokana na zile sababu zilizoko kwenye jamii ikiwemo hofu ya kutoaminiwa, kubaguliwa na hata uwezekano wa kushambuliwa. Hali ni mbaya zaidi karibu katika maeneo yote ambayo MSF inafanya kazi kama vile maeneo yenye mizozo, ambako hakuna ulinzi kwa waathirika, kiwango kikubwa cha vurugu za jumla na wahusika kutoshtakiwa na pia ambako watu mara nyingi hutegemea msaada kutoka nje. Idadi na jiografia ambako wafanyakazi wetu wanatoka kunahitajika juhudi endelevu za kutoa taarifa na kueneza uelewa kuhusu sera za MSF katika matukio ya udhalilishaji na kubugudhiwa pamoja na kuweka miundombinu itakayowezesha upatikanaji wa utoaji wa taarifa kuhusu udhalilishaji na kubugudhiwa.

Kufanikisha na kuendelea kukidhi vigezo vya mazingira ya kazi yaliyo huru kutokana na vitendo vya bugudha na udhalilishaji ni jambo endelevu ambalo sote kwa pamoja tunawajibika. Pia tumejihakikishia kutofanya vitendo vya kuwadhuru watu walio kwenye mazingira magumu ambao tunapambana kuwasaidia.

Taarifa kuhusu mabadiliko ya takwimu: Kutokana na kuboreshwa kwa mfumo wa ukusanyaji taarifa, MSF imeboresha takwimu zake kwa mwaka 2017. Kwa muktadha huo, jumla ya idadi ya malalamiko katika mwaka 2017 imegundulika kuwa yalikuwa ya kiwango cha juu kuliko ilivyoripotiwa awali: Kulikuwa na kesi 182 tofauti na 146 zilizorekodiwa; idadi ya kesi zilizothibitishwa mwaka 2017 pia ziliongezeka kiasi. Tafadhali kumbuka kuwa baadhi ya kesi zilizoripotiwa kwa mwaka 2018 bado zinaendelea kufanyiwa uchunguzi, kwa hivyo takwimu za jumla huenda zikabadilika kidogo.

Change country