Shirika la MSF lina miradi yake mikubwa katika nchi za ukanda wa Afrika Mashariki ikiwemo Sudan Kusini, Kenya, Tanzania, Uganda, Ethiopia, Somalia na Burundi. Katika nchi hizi, MSF inasimamia hospitali, vituo vya afya na kliniki zinazotembea na kuzindua miradi ya dharula wakati huu mahitaji ya huduma za afya yakiongezeka.
MSF pia ina ofisi za kanda nchini Kenya, ambapo inasaidia miradi ya matibabu nchini humo na kwenye nchi zinazozunguka, inaajiri wafanyakazi kusaidia kuratibu operesheni zake duniani kote na kueneza uelewa kuhusu majanga ya kibinadamu ambayo tunashughulikia. MSF pia inakitengo maalumu cha ubunifu, kitengo maalumu cha dharula ambacho kinasaidia miradi yetu duniani pamoja na usambazaji katika vituo vya nchini Kenya.