Skip to main content

Newsletter block in header

prev
next

You are here

Historia 

 

MSF ilianzishwa nchini Ufaransa mwaka 1971 na kikundi cha madaktari na waandishi wa habari ambao walitaka kutoa msaada wa matibabu na kujadiliana kuhusu madhila waliyoshuhudia wakati wakitekeleza majukumu yao. 

 Lengo lao lilikuwa kuanzisha shirika huru ambalo linalenga kutoa msaada wa matibabu ya dharura haraka. Watu mia tatu walijitolea wakati shirika ilianza, wakiwa madaktari, wauguzi na wafanyikazi wengine, pamoja na wale madaktari na waandishi wa habari 13 walioanzisha MSF. 

MSF iliundwa kwa imani kwamba watu wote wanapaswa kupata huduma ya afya bila kujali jinsia, rangi, dini, imani au ushirika wa kisiasa, na kwamba mahitaji ya kimatibabu ya watu inazidi heshima mipaka ya kitaifa. Kanuni za hatua za MSF zinaelezewa katika hati yetu, ambayo ilianzisha mfumo wa shughuli zetu.

Leo hii, MSF ni vuguvugu la kidunia la zaidi ya watu  67,500  wanaofanya kazi katika nchi 70.