Skip to main content

Newsletter block in header

prev
next

You are here

Hati na Kanuni

Misingi yetu

Kiini cha utambulisho wetu ni kufanya kazi kwa uhuru, uadilifu na kutofungamana na upande wowote.

Misingi hii ndio imekuwa ikituongoza katika ufanyaji kazi wetu – kuanzia kwenye kutoa huduma za matibabu, fedha, usafiri na mawasiliano – tangu MSF ilipoanzishwa miaka 45 iliyopita. Na nikupitia mawazo haya na mchango chanya wa shirika letu, tulitambuliwa mwaka 1999 ambapo MSF ilitunukiwa tuzo ya Amani ya Nobel.

Tuko Huru

Ni nadra sana tunapokea msaada wa kifedha kutoka kwa Serikali, wafanyabiashara au taasisi nyingine kwaajili ya kazi zetu, badala yake tunategemea sana ukarimu wa watu zaidi ya milioni tano duniani kote. Zaidi ya asilimia 95 ya kipato chetu kinatoka kwa wafadhili binafsi ambao wamekuwa wakituchangia mara kwa mara na kiasi kidogo kusaidia kazi zetu.

Hii inamaana kuwa pale panapokuwa na dharula, hatuhitaji kusubiri fedha kutolewa au kwa vyombo vya habari kutusaidia kuhamasisha; tunaweza kufanya kazi kwa uharaka kuokoa maisha ya watu kule ambako kuna janga la kibinadamu na kunahitajika msaada wa matibabu.

Uhuru wetu wa kifedha unamaana kuwa msaada tunaotoa hauwezi kutumika kusaidia shughuli za kisiasa za Serikali au malengo ya kijeshi.

Sisi ni Waadilifu

Tunatoa huduma za matibabu bure kwa watu wanaohitaji. Haijalishi ni nchi gani wanatokea, dini gani wanayoamini au kutokana na itikadi zao za kisiasa. Kile tunachojali ni kuwa wote ni binadamu wanaohitaji msaada ambao tunautoa.

Hatupendelei

Katika maeneo yenye mizozo hatuegemei upande wowote, lakini tunaenda kule ambako watu wanauhitaji zaidi. Katika wodi za hospitali za MSF, unaweza kukuta raia waliojeruhiwa sambamba na wanajeshi waliojeruhiwa kutoka upande mwingine. Kila kituo cha afya cha MSF hakina alama yoyote ya bunduki mlangoni, zana na silaha nyingine zinapaswa kuachwa getini, tunatengeneza mazingira ya haki ambayo kila mtu anayehitaji huduma anaweza kupewa.

Katika kuelezea ari yetu ya kutofungamana na upande wowote tunakofanya kazi ni suala la muhimu na ndio maana tumeruhusiwa kutoa msaada wa matibabu katika maeneo ambayo mazingira yake yanachangamoto duniani.

Tunatumia sauti yetu kuwasaidia wagonjwa

Pamoja na kuokoa maisha ya watu kwa kutoa msaada wa matibabu, MSF inazungumza kwa niaba ya wagonjwa wetu, kusaidia kueneza uelewa kuhusu madhila ambayo tunashuhudia katika maeneo ambayo tunafanya kazi.

Wakati tukipokea tuzo ya Amani ya Nobel mwaka 1999, rais wa zamani wa MSF, Daktari James Orbinski, alisema: ‘Hatuna uhakika kwamba wakati wote maneno yanaweza kuokoa uhai, lakini tunajua fika kuwa ukimya unaweza kuua’.

Tunaweza kuzungumza hadharani au katika maeneo ya siri kwa lengo la kuepusha madhila na kuokoa maisha.

Uwajibikaji na Uwazi

Tunachukua jukumu kuwa na uwazi katika matendo na maamuzi yetu.  Majadiliano na  uchambuzi wa kazi tunayoifanya na pia masuala pana ya kibinadamu ni muhimu katika uboreshaji wa kazi yetu.