Je unavutiwa kusaidia miradi ya tiba ya MSF? Kila mwaka zaidi ya wafanyakazi wa kimataifa 3,800 wanaunganisha nguvu na ujuzi kuungana na wafanyakazi kutoka mataifa mengine zaidi ya 39,000 ambapo tunafanya kazi za kutoa huduma za matibabu kwa wale ambao wana uhitaji mkubwa.
Wafanyakazi wetu wanafanya kazi nyakati za mizozo na milipuko ya magonjwa, na pia ikitokea majanga ya asili, mazingira huwa ya changamoto lakini matokeo yake ni makubwa.
Tunahitaji wafanyakazi madaktari na wasio madaktari ili kufanya kazi yetu kuwa rahisi. Je unafikiri una uwezo? Tazama zaidi ni akina nani tunawatafuta, miiko ya kazi na namna ya kuomba kazi hapa chini.