"Mpaka kufikia Februari 14, kulikuwa na kesi 64,000 za COVID-19, asilimia 99 ya kesi hizi zikiripotiwa China,” anasema Gert Verdonck, Mratibu wa misaada ya dharura wa MSF kwaajili ya COVID-19. “Vifaa kinga ni muhimu. Kahivyo tunataka kuchangia kusaidia wafanyakazi walio mstari wa mbele kwa kuwa na vifaa maalumu ambayo wanavihitaji kwa usalama wao hasa wakati huu wa mlipuko mkubwa kama huu.”
Ukiwa na uzito wa tani 3.5, vifaa hivi vimetolewa katika kituo chetu cha usambazaji mjini Brussels; Ubeligiji kupitia shirikisho la misaada la Hubei, ili kufika katika hospitali ya Wuhan Jinyintan, moja ya hospitali ambazo ziko mstari wa mbele kuwatibu wagonjwa wa COVID-19.
Timu ya MSF kwenye mji wa Hong Kong ilianzisha mradi mwishoni mwa mwezi Januari ukilenga kutoa elimu ya afya kwa watu walio katika mazingira magumu. Ushirikishwaji wa jamii ni suala muhimu katika hali ya mlipuko wowote na kwenye mji wa Hong Kong, tunalenga makundi maalumu ambayo yanauwezekano kuwa hayana uwezo wa kupata taarufa za tiba, kama vile athari za kijamii na kiuchumi. Timu hii pia inawalenga watu ambao wako hatarini kuumwa zaidi ikiwa wataambukizwa, kama vile wazee.
“Timu yetu tayari imeshafanya mahojiano ya vipindi vya ana kwa ana na wafanya usafi wa mitaa, wakimbizi na waomba hifadhi na wale wasioona katika siku za hivi karibuni,” anasema Karin Huster, ambaye ni kiongozi wa mradi huu mjini Hong Kong. “Tunabadilishana taarifa mpya, taarifa za kitabibu zilizothibitishwa, lakini zaidi na pengine kwa umuhimu, tuke kule kuwasikiliza na kujibu maswali mengi ambayo ugonjwa hu umeyasababisha. Hofu mara nyingi huenea kwa haraka kuliko virusi, kwa hivyo kuwasaidia watu kudhibiti msongo na hofu ni jambo la muhimu sana kwetu.”
Zaidi, MSF unatuma mchango wa karibu tani moja ya vifaa kinga katika kituo cha huduma za magari ya wagonjwa cha Hong Kong St John, kuwasaidia kufanya shughuli zao hadi pale hazina yao itakapokuwa sawa tena. Wafanyakazi hawa wanawasafirisha wagonjwa hatari, na hivyo, ni muhimu sana kuhakikisha wanapata vifaa kinga maalumu kwa ulinzi wa kazi yao.
Na tena, katika nchi nyingine, MSF inakofanya shughuli zake, timu zinajiandaa ikiwa kutatokea mlipuko wa COVID-19. Katika nchi kadhaa, hasa katika eneo la nchi za Kusini na kusini mashariki mwa Asia, MSf inawasiliana na mamlaka za afya na kuahidi kutoa usaidizi pale watakapohitajika. Hii ikiwemo mafunzo kwa wafanyakazi wa afya kuhusu namna ya kuzuia maambukizi na njia za kudhibiti na elimu ya afya kwa makundi yaliyoko hatarini, ikifanana kabisa na shughuli ambayo MSF ilifanya mwaka 2003 wakati wa mlipuko wa homa ya mafua ya SARS, iliyokuwa inasababishwa na aina kama hii ya virusi vya Corona.