© Agnes Varraine-Leca/MSF
COVID-19 Coronavirus

Kujiandaa kwa madhara ya COVID-19

Utawezaje kuosha mikono yako mara kwa mara wakati hauna maji wala sabuni? Unawezaje kuweka nafasi kati yako na mtu mwingine ikiwa unaishi katika maeneo ya msongamano au kambi ya wakimbizi? Namna gani utaweza kuacha kuvuka mpaka ikiwa unakimbia vita? Ni namna gani wale walio na magonjwa mengine wanazeza kuchukua hatua zaidi kujikinga wakati hawawezi hata kufika hospitali?

Kila mtu ameathirika kutokana na mlipuko wa COVID-19, lakini athari zake zinaweza kusikiwa na wachache na wengine zaidi.

Wakati ugonjwa wa COVID-19 ukienea zaidi, utaendelea kuonesha mgawanyiko uliopo baina ya mifumo yetu ya afya. Utaonesha kutengwa kwa baadhi ya makundi katika kupata huduma, ama kutokana na hadhi yao ya kisheria au kwa sababu nyingine ambazo zinawafanya kuwa walengwa za muhimili. Utaonesha uwekezaji finyu katika mfumo wa afya kwa wote, hii ikiwa na maana kuwa kwa baadhi ili kupata huduma kutatokana na nguvu ya kipato na sio uhitaji wa matibabu. Utaonesha mapungufu ya serikali – sio tu kwa huduma za afya – kupanga utoaji huduma ambao utafikia mahitaji ya kila mtu. Utaonesha tishio la maisha linalotokana na watu kukosa makazi, machafuko, umasikini na vita.

Watu ambao watataabika sana watakuwa ni wale ambao wametengwa tayari – kutokana na ubanaji matumizi, waliokimbia kutokana na vita, wale ambao hawana uwezo wa kupata matibabu kutokana na hali ya kubinafsishwa kwa huduma wa afya. Na pia itakuwa kwa wale ambao hawana uwezo wa kuhifadhi chakula cha kutosha na ambao hawawezi kupata mlo wa usiku kila wiki, wale ambao wanalipwa kidogo, wanaofanyishwa kazi sana na kunyimwa likizo ya ugonjwa, hawawezi kufanya kazi nyumbani – na wale walionaswa kwenye maeneo yenye mizozo wakilengwa na mabomu na mashambulizi ya mara kwa mara.

Na namna gani unaweza kuwatibu wagonjwa bila ya kuwa na mahitaji yote? Mifumo mingi ya afya inajiandaa kwa madhara ya COVID-19 na ambayo tayari yanashuhidia madhila ya vita, hali tete ya kisiasa, matumizi mabaya ya rasilimali, rushwa, ubanaji matumizi na vikwazo. Hata sasa hazina uwezo wa kwenda na hali ya wagonjwa wachache walionao.

COVID-19 inabainisha namna gani maamuzi ya sera yanavyotenga watu, kupunguza upatikanaji wa huduma bure za afya na kuongeza ombwe ambalo sasa linasikiwa na kila mmoja wetu. Sera hizi nik adui wa afya shirikishi.

Wakati huu MSF ikiendelea kukabiliana na mlipuko wa COVID-19, tutajikita zaidi kwa watu walio katika mazingira hatarishi na wamesahaulika. Tumeanza kufanya kazi Hong Kong mwanzoni mwa mwaka huu katika kushughulikia kisa cha kwanza cha mgonjwa wa COVID-19, na sasa tuna timu ya wataalamu wetu waliopelekwa kwenye kitovu cha mlipuko nchi ya Italia. Tutaendelea kuongeza wigo wa kazi zetu kwa kila namna tutakayoweza kuukabili mlipuko huu.

Hata hivyo, kuna maamuzi ambayo yanaweza kufanyika sasa ambapo yatapunguza makali ya janga tarajiwa ambalo jamii nyingi zitakabiliwa nalo. Msomgamano wa watu katika visiwa vya Ugiriki watu wanahitaji kuondolewa. Hii haimaanishi kuwarudisha watu Syria ambako vita bado iko. Ina maanisha kutafuta njia kuwahusiaha watu hawa katika jamii ambapo watakuwa na uwezo wa kuchukua tahadhari kama vile kutengeneza nafasi kati ya mtu na mtu na kujitenga.

Kadhalika, vifaa vinapaswa kugawiwa katika maeneo yote kulingana na mahali vinakohitajika zaidi. Hii itahitaji kuanza na mataifa ya Ulaya kubadilishana vifaa na Italia. Na hivi karibuni itahitajika kupelekwa kwenye maeneo zaidi yaliyoathirika na mlipuko na ambayo uwezo wake wa kukabiliana na mlipuko umetatizika.

Kama MSF tutahitajika kudhibiti ombwe la miradi yetu ambayo inaendelea kutekelezwa. Utoaji tiba wa ugonjwa wa Surua nchini DRC unahitajika kuendelea. Sawa na kutoa misaada ya dharura kwa jamii zilizoathirika na vita Cameroon au Jamhuri ya Afrika ya Kati. Hizi ni baadhi ya jamii ambazo kamwe hatuwezi kuziangisha. Kwao, mlipuko wa COVID-19 ni shambulio jingine la maisha yao.

Mlipuko huu unaonesha udhaifu wetu wa jumla. Kutokukosa nguvu ambako kila mtu anajisikia hivi leo, mpasuko wa hisia kuhusu usalama, hofu kuhusu mustakabali wetu. Hizi zote ni hofu na wasiwasi unaosikiwa na watu jamii nyingi ambazo zilikuwa zimetengwa, kusahaulika au kushambuliwa na wale walioko madarakani.

Ni imani yangu kuwa COVID-19 sio tu itatufundisha kuosha mikono yetu, lakini kuzifanya serikali kuelewa kuwa huduma za afya ni kwa wote.