Athens, 12 Machi 2020 – Idadi kubwa ya watu kupita uwezo na hali ngumu ya maisha katika kisiwa cha Ugiriki, kunatoa upenyo kutokea kwa gharika ya maambukizi ya COVID-19, limeonya shirika la Madaktari Wasio na Mipaka MSF.
Kutokana na ukweli kuwa hakuna huduma muafaka za usafi na ukomo wa huduma za afya, hatari ya virusi kuenea miongoni mwa wakazi wa kwenye makambi ni ya kiwango cha juu punde tu wakiambukizwa. Na wakati huu kisa cha kwanza kikiripotiwa kwa Lesbos, raia wa Ugiriki, kuwahamisha wakazi wa kambi hiyo kunahitajika wakati huu kuliko wakati mwingine wowote.
“Kweye baadhi ya maeneo ya kambi ya Moria kuna bomba moja tu la maji kwa watu karibu1,300 na hakuna sabuni. Familia za watu watano au sita wanapaswa kulala katika eneo ambalo halizidi mita 3. Hii ina maanisha kuwa ile njia inayopendekezwa kama yakunawa mikono mara kwa mara na kuepuka kugusana au kushikana mikono kuzuia kuenea kwa maambukizi ni wazi haiwezekani”, anaeleza Dr Hilde Vochten, mratibu wa matibabu wa MSF nchini Ugiriki.
Duniani kote serikali zinatangaza kufuta matukio na kuzuia mikusanyiko ya idadi kubwa ya watu, lakini katika kambi ya kisiwa cha Ugiriki watu hawana jinsi zaidi ya kuendelea kuishi huko. Afya yao iko hatarini. COVID-19 inaweza kuwa ni tishio jingine watu wanalokabiliana nalo hapa, lakini hali wanayoishi kwa sasa inawaweka hatarini zaidi kuliko hata watu wengine.
“Tunawasiliana na taasisi ya kitaifa ya afya ya uma ili kuratibu shughuli za kufanya, ikiwemo taarifa za kiafya na udhibiti wa ugonjwa kwa wenyeji na waomba hifadhi pia”, aliongeza Dr Vochten. “Lakini tunapaswa kuwa wa kweli: itakuwa ngumu kudhibiti mlipuko wowote katika kambi zilizoko Lesvos, Chios, Samos, Leros na Kos. Mpaka leo hii hatujaona mpango wowote wa msaada wa dharura kuwalinda na kuwatibu watu wanaoishi huko ikiwa kutakoea mlipuko”.
Kile kinahitajika kutoka kwa mamlaka za afya ni mpango ambao utajumuisha hatua za udhibiti wa maambukizi, uhamasishaji afya, utambuzi wa haraka wa mgonjwa, kutenga na udhibiti wa magonjwa mengine pamoja na kutoa matibabu ya wagonjwa mahtuti.
Ikiwa hivi vyote havipo, kuwahamisha watu kutoka kwenye kambi za wakimbizi katika visiwa vya Ugiriki ni suala linalohitajika kufanyika sasa kuliko wakati mwingine wowote. Kuwalazimisha watu wasalie kwenye maeneo yale kwa sababu tu ya mikakati ya nchi za Ulaya kudhibiti wahamiaji, lilikuwa ni suala la kutowajibika, lakini inaelekea kuwa uhalifu ikiwa hakuna hatua zozote zitakazochukuliwa kuwalinda watu.
Kuna waomba hifadhi zaidi ya 42,000 katika maeneo matano ya visiwa vya Ugiriki. Wakati huu wito wa kutaka watu kuondolewa kutokana na mlipuko huu ukionekana unaogopesha, kuwalazimisha watu waishi katika msongamano kama ule, bila ulinzi, unaelekea kuwa jinai. Serikali ya Ugiriki na nchi wanachama za umoja wa Ulaya ni lazima zichukue hatua haraka na kuwahamisha wahamiaji wengi na kuwapeleka maeneo salama kabla ya kuja kujutia baadae.