Timu ya shirika la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) nchini Italia inatoa msaada kwa mamlaka za afya kukabiliana na mlipuko wa virusi vya Corona COVID-19. Wafanyakazi wa MSF wako katika hospitali nne wa majimbo ya kaskazini kama vile Lodi, sehemu ya jimbo la Lombardy eneo ambalo lilikuwa kitovu cha mlipuko nchini humo.
Timu ya MSF iliyoko kwenye jimbo la Lodi inaundwa na mtaalamu wa magonjwa ya kuambukiza, mchoma sindao ya usingizi, wauguzi na watu wa ugavi, ambao wanaleta uzoefu wa dunia katika kudhibiti milipuko kutoka katika hospitali ambazo MSF inasaidia hospitali za Italia. Wafanyakazi wa MSF wanafanya kazi kwa kushirikiana na mamlaka za afya za ndani na wafanyakazi wengine katika miji ya Lodi, Codogno, Casalpusterlengo na Sant’Angelo Lodigiano katika shughuli mbalimbali, ikiwemo kuzuia maambukizi na kuwahudumia wagonja.
Nyongeza ya wafanyakazi kwenye mji wa Codogno wanaweza kuhudumia watu katika vitanda 20 vilivyopo, ambavyo vimekuwa havitumiki kutokana na uhaba wa wafanyakazi. Timu ya MSF itafanya kazi sambamba na madaktari na wauguzi kutoka vitengo tofauti na kwa pamoja watatoa huduma kwa wagonjwa wa COVID-19.
“Tumekutana na madaktari na wauguzi kwenye jimbo la Lodi ambao wamekuwa wakifanya kazi bila kuchoka kwa majuma kadhaa na katika mazingira ya changamoto sana,” anasema Dr Claudia Lodesani, mtaalamu wa magonjwa ya kuambukiza na rais wa MSF nchini Italia, ambaye anaratibu timu inayokabiliana na COVID-19 nchini Italia. “Tunatoa msaada kuwasaidia kwa kuwa wana uhitaji mkubwa na kwa hospitali zilizozidiwa uwezo katika kukabiliana na mlipuko huu, ili waweze kuwahudumia wagonjwa vizuri.”
Msaada wa magonjwa ya kuambukiza utasaidia utekelezaji wa hatua za kuzuia na kudhibiti shughuli ambazo tayari zimeanza kutekelezwa ndani ya hospitali zenyewe, kuepuka maambukizi ya virusi na kutoa hakikisho la usalama kwa wafanyakazi wa afya.
“Katika mlipuko wa aina hii, kuzuia maambukizi ya virusi ni suala la muhimu sana. Katika hospitali ni muhimu kupunguza hatari kwa wafanyakazi walio mstari wa mbele, suala la muhimu kupambana na mlipuko huu,” anasema Dr Lodesani. “Nje, kila mtu anapaswa kuheshimu maelekezo ya wizara ya afya, ili kuzuia maambukizi na kuepusha athari kwa hospitali ambazo mara kwa mara zinahitaji kuendelea kutibu watu kutokana na maradhi au majeraha.”
MSF imetoa usaidizi kwa timu inayokabiliana na mlipuko huu nchini Italia kama moja ya nchi zilizoathirika pakubwa na COVID-19. Timu zetu zinafanya kazi kwa kushirikiana na watu wa Italia na wafanyakazi wa afya ambao wako mstari wa mbele kumaliza mlipuko huu. MSF pia inawasiliana kwa karibu na mamlaka za afya kwenye nchi nyingine ambako inafanya kazi, katika kutibu COVID-19. Kwa kuzingatia ukubwa wa tatizo la mlipuko, uwezo wa MSf kusaidia nchi zaidi unategemea aina ya mlipuko na pia uwezo wa kutuma watu.