No patents
Access to medicines

MSF inatoa wito wa kutoweka umiliki au kujinufaisha kutokana na dawa za COVID-19, majaribio na chanjo wakati wa mlipuko

27 Machi 2020 -   Shirika la kimataifa la Madaktari Wasio na Miapaka, MSF, leo hii linatoa wito wa kutokuwa na umiliki au kujinufaisha kutokana na dawa, majaribio au chanjo itakayotumika kwaajili ya mlipuko wa COVID-19, na serikali kujiandaa kufuta na kuchukua haki miliki pamoja na kuchukua hatua nyingine kama vile udhibiti wa bei, kuhakikisha upatikanaji, kupunguza bei na kuokoa maisha zaidi ya watu.

Tayari nchi za Canada, Chile, Ecuador na Ujerumani zimeshachukua hatua kuhakikisha inakuwa rahisi kuchukua umiliki kwa kutoa leseni ya lazima kwa dawa za COVID-19, chanjo, na vifaa vingine vya matibabu. Hivyohivyo, serikali ya Israel imetoa leseni ya lazima kwa haki miliki ya dawa zinazochunguzwa kwa matumizi ya COVID-19.

Baada ya ukosolewaji mkubwa kutoka kwa mashirika ya kiraia na MSF, kampuni ya kutengeneza dawa ya Gilead ilitoa kibali maalumu kutoka kwa shirika la Marekani la udhibiti wa chakula na dawa ambapo itaruhusu kuongezwa kwa muda wa miaka 20 kwa hati miliki iliyotoa kwa mataifa zaidi ya 70 duniani kama dawa ya majaribio kutibu ugonjwa wa COVID-19, remdesivir. Matokeo ya awali ya majaribio ya kitabibu ya remdesivir kutibu ugonjwa wa COVID-19 yanatarajiwa kutolezwa mwezi April. Hata hivyo kampuni ya Gilead bado haijathibitosha ikiwa itatoa kibali hicho cha hati miliki kwa mataifa zaidi.

“Gilead haina biashara ya faida kutokana na mlipuko huu na ni lazima ithibitishe kuwa haitadai haki miliki au haki nyingine,” anasema Dana Gill, mshauri wa masuala ya sera wa MSF. “Vinginevyo, Gilead inajitengenezea mazingira ya kutaka kutoza kiasi chochote itakachojisikia cha dawa ya remdesivir wakati wa janga hili la kidunia, na kwa miaka mingi ijayo. Hii inakasirisha zaidi ukizingatia kiwango kikubwa cha kodi wa walalahoi na rasilimali za uma ambazo tayari zimetumika katika utafiti na kutengeneza dawa ya remdesivir.”

MSF inaguswa na upatikanaji wa dawa nyingine siku za usoni, majaribio na chanjo kwa ajili ya COVID-19 katika maeneo ambayo MSF inafanya kazi na katika mataifa mengine ambayo yameathirika na mlipuko huu, na inatoa wito kwa serikali kuandaa mpango wa kufuta aua kuchukua haki miliki ya dawa ya COVID-19 kwa kutoa leseni ya lazima. Kuondoa umiliki binafsi na vikwazo vingine ni muhimu kusaidia kuhakikisha kuwa kuna upatikanaji wa kutosha na kuuzwa katika bei ambayo kila mmoja atakuwa na uzewo wa kununua,

“Tunajua sana kutokana na kazi zetu ulimwenguni ina maana gani kwetu sisi kuwahudumia watu kwa sababu tu dawa wanayohitaji ni ya aghali au haipatikani,” anasema Dr Marcio da Fonseca, mshauri wa magonjwa ya kuambukiza wa MSF. “Katika nchi ambazo makampuni ya dawa yanaweka haki za umiliki, tunatoa wito kwa serikali kutengeneza sheria itakayobatilisha haki miliki hizo ili kuhakikisha dawa zinapatikana katika gharama nafuu ili kuokoa maisha zaidi.

Kampuni ya majaribio ya Marekanim Cepheid inatoa mfano mwingine mzuri wa kampuni zinazotaka kutengeneza faida kupitia mlipuko huu. Kampuni hiyo imepokea kibali cha dharura cha kufanya majaribio ya dawa (Xpert Xpress SARS-CoV-2) mpango utakaotoa matokeo ndani ya dakika 45, kwa kutumia mashine zilizopo ambazo zimekuwa zikitumika kwa ajili ya ugonjwa wa kifua kikuu Tb, HIV na magonjwa mangine.

Cepheid tayari imetangaza kuwa itatoza kiasi cha dola wa Marekani 19 kwa kila jaribio kzenye nchi zinazoendelea, zikiwemo nchi masikini zaidi duniani ambazo raia wake wanaishi chini ya dola mbili kwa siku. MSF pamoja na tafiti nyingine kuhusu majaribio ya TB ya kampuni ya Cepheid (ambayo inatumia aina ile ile ya mashine kwaajili ya TB na ambapo kampuni hii inatoza dola 10 katika nchi zinazoendelea), inaonesha kuwa gharama ya bidhaa, ikiwemo uzalishaji, na gharama nyingine, kwa kila kipimo ni chini ya dola 3 na hivyo basi kila jaribio lingeweza kuuzwa kwa faida ya dola 5.

“Wakati huu mlipuko ukishika kasi, huu sio muda wa kujaribu bei kubwa katika soko ambayo itakubalika,” anasema Stijn Deborggraeve, mshauri wa masuala ya utambuzi wa kampeni za MSF. “Tunajua ni muhimu kiasi gani kufanyika majaribio katikati ya mlipuko huu, kwa hivyo majaribio lazima yawe rafiki katika nchi zote.”

MSF inaonya kuwa, bei kubwa na ubinfasi utasababisha kuwepo kwa mgao wa dawa, majaribio na chanjoi, jambo ambalo litasababisha mlipuko huu kuendelea.

“Makampuni ya dawa na upimaji wanachagua kuwa sehemu ya tatizo kuliko kuwa sehemu ya suluhu, yakionesha kuwa hata katika kipindi hiki cha janga la kiafya, hawatafanya kitu sahihi,” anasema Gill. “Tunatoa wito kwa serikali kutambua ni maisha ya watu wangapi yako hatarini na kutumia nguvu zake kutengeneza dawa, majaribio na upatikanaji wa chanjo na ambazo kila mtu ataweza kupata.”