MSF has started an intervention for the outbreak of COVID-19
COVID-19 Coronavirus

Virusi vya Corona: Nini MSF inafanya?

Mahojiano na Clair Mills, Mkurugenzi wa tiba wa MSF.

Je tuko sahihi kuuogopa ugonjwa wa COVID-19?

Kuna viashiria kadhaa ambavyo vinaufanya ugonjwa huu uogopeshe. Kuwa tu ni virusi vipya, hakuna kinga iliyopo; zaidi ya chanjo 35 zinazodaiwa kuwa na uwezo wa kutibu virusi hivi ziko kwenye majaribio ya maabara, lakini wataalamu wanakubaliana kuwa hakuna chanjo iliyopo inayoweza kutumika katika muda wa miezi 12 hadi 18. Idadi ya vifo, ambayo kiujumla inahesabiwa kwa kuzingatia utambuzi wa wagonjwa na hivyo inakuwa ngumu kukadiria kwa uhakika, ila inaonekana kuwa asilimia 1. Inafahalika kuwa angalau wale walioathirika wanaweza kusambaza ugonjwa kabla ya kuonesha dalili – au hata pale wanapokuwa hawana dalili zozote. Kwa ziada, kuna idadi kubwa angalau ya asilimia 80 ya watu wanaonesha dalili kidogo sana za ugonjwa huu, jambo ambalo linaleta ugumu kuwatambua na kuwatenga kwa haraka. Utambuzi wa ugonjwa unahitaji vipimo vya maabara au vipimo vya picha ambavyo hupatikana kwenye maeneo yaliyoendelea na yenye utaratibu mzuri. Hivyo basi haishangazi kuona kuwa ni vigumu kudhibiti virusi hivi visienee, ambapo sasa viko katika nchi zaidi ya 100 duniani. Mlipuko huu bado pia ni tofauti sana na ile ya Surua, kipindupindu, au Ebola – ambapo Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka limeweza kuwa na ujuzi navyo katika muda wa miongo kadhaa iliyopita.

Zaidi, leo hii inakadiriwa kuwa asilimia 15 hadi 20 ya wagonjwa wenye COVID-19 wanahitaji kulazwa hospitalini na asilimia 6 wanahitaji uangalizi wa karibu wa kati ya wiki 3 hadi 6. Hili linawezekana ikiwa tu mfumo wa afya utabadilishwa – hii ilikuwa wazi nchini China wakati mlipuko ulipoanza, na sasa inashuhudiwa Italia. Kwa sasa kuna wagonjwa 1,100 ambao wamelazwa katika wodi za wagonjwa mahututi na mfumo wa afya kaskazini mwa nchi hiyo, licha ya kuwa ni wa kiwango cha juu, umezidiwa kutokana na kuongezeka kwa kasi kwa idadi ya wagonjwa.

Kama ilivyo ada wakati wote wa mlipuko kama huu, wahudumu wa afya wenyewe wako hatarini kuambukizwa. Kati ya katikati ya mwezi Januari na Februari, nchini China wafanyakazi zaidi ya 2,000 waliambukizwa virusi vya Corona (Asiliamia 3.7 wote ni wagonjwa).

Mlipuko huu ni wazi huenda ukasababisha athari kubwa katika mifumo ya afya na vituo vya dharura, kutotilia umakini kwa magonjwa mengine yanayohatarisha maisha ya watu na kwa magonjwa mengine sugu mahali kwingine…lakini zaidi ni kwa nchi zinazoendelea ambako mifumo ya afya si thabiti.

 

Baadhi wanahisi kuwa namna ugonjwa huu unavyoshughulikiwa umepewa umuhimu ambao haustahili, na kwamba dawa, kufunga mipaka, kuwatenga watu, n.k – huenda ikawa ni mbaya zaidi kuliko ugonjwa wenyewe. Je hili lina uhalali? 

Licha ya kuwa hawawezi kuzuia mlipuko usiendelee kuenea, hatua ambazo zinaendelea kuchukuliwa kwa sasa na mataifa mengi zinaweza kupunguza kasi kwa kupunguza ongezeko la kesi na kuweka ukomo wa watu walio na hali mbaya, ambapo mfumo wa afya unalazimika kudhibiti kwa wakati huohuo. Lengo sio tu kupunguza idadi ya kesi lakini pia kuzuia kuenea zaidi, kuepuka misongamano katika hali ya dharura na vitengo vya wagonjwa mahututi.

 

Ni vipi vipaumbele vya MSF katika hali hii, na hofu yake ni nini?

Vipaumbele vya kushughulikia suala kama hili vinatofautiana kutoka hali moja kwenda nyingine.

Katika maeneo ambayo leo hii yanaonekana kunusurika, kama vile Jamhuri ya Afrika ya Kati, Sudan Kusini na Yemen, ambako vita vimeshamiri au kwenye maeneo ambayo mifumo ya afya inashambuliwa bado wanakabiliana na changamoto ya kufikia kiwango cha mahitaji ya raia wake, ni muhimu sana kuwalinda wafanyakazi wa afya na kupunguza kasi ya kuenea kwa maambukizi kadiri inavyowezekana. Hili linafanyika kwa kutekeleza miradi ya kuzuia – kubaini maeneo hatarishi yenye watu wengi; kueneza uelewa na kusambaza taarifa; kusambaza sabuni na vifaa kinga kwa wafanyakazi wa afya; na kuweka mifumo mizuri ya usafi katika maeneo ya sekta za afya – kuzuia hospitali zetu na kliniki kuwa maeneo ya vyanzo vya kusambaza magonjwa. Katika mataifa haya ambayo MSF imekuwepo kwa muda mrefu tunataka kuchangia juhudi hizi dhidi ya COVID-19 huku tukihakikisha kunakuwa na uendelevu katika kutibu Malaria, Surua, magonjwa ya mfumo wa hewa n.k.

Uendelevu huu umedumazwa na vikwazo (zuio la kuingia nchini, kuwatenga watu kwa siku 14, n.k)  vilivyowekwa na Serikali kwa wafanyakzi kutoka baadhi ya nchi fulani kama vile Ufaransa na Japan….ambako baadhi ya wafanyakzi wetu wa kimataifa wanatokea, pamoja na kufungwa kwa mipaka na kufutwa kwa baadhi ya safari za anga. Licha ya vikwazo hivi, nguvu yetu iko kwenye ukweli kuwa tinategemea wafanyakazi kutoka kwenye nchi husika. Wanawakilisha asilimia 90 ya wafanyakazi wetu walioko kwenye maeneo ya kazi.

Katika nchi ambazo mifumo ya afya iko imara lakini mlipuko ukiwa kwa kiwango cha juu, kama vile Italia au Iran, changamoto kubwa ni kuepuka msongamano mkubwa katika hospitali.

Katika hali hii tunaweza kuchangia juhudi za kuwa na timu ya madaktari wa kitaifa kuhakikisha wafanyakazi wa MSF wanapatikana kusaidia au kuwapumzisha pale inapohitajika. Tunaweza tu kusaidia kwa kutoa uzoefu wetu wa kutibu na udhibiti wa maambukizi unaohitajika wakati wa mlipuko. Tumetoa timu ya watu kusaidia hospitali nne kaskazini mwa Italia na pia tumetoa usaidizi kwa Serikali ya Iran kuwahudumia wagonjwa mahututi. Kwa kutegemea maendeleo ya mlipuko nchini Ufaransa, tutahakikisha uzoefu unapatikana, uratibu na ujuzi wa wafanyakazi wetu, ikiwa watakuwa msaada.

Kiungo kimoja muhimu katika vita dhidi ya COVID-19 ni upatikanaji wa vifaa kinga, hasa maski na glovu zinazotumiwa wakati wa matibabu hospitalini. Ukadiriwaji wa uhaba wa vifaa hivi kunafanya majimbo mengi yawe na uhitaji mkubwa, jambo ambalo linaweza kuwa kioo katika baadhi ya majimbo kwa kujaribu kuhodhi vifaa kinga. Katika hali ya sasa vifaa hivi vinapaswa kutazamwa kama uhitaji wa lengo la pamoja vitumike vizuri na kwa mahitaji na hivyo wafanyakazi wa afya walioko mstari wa mbele wawe kipaumbele, popote pale walipo duniani.

Kiujumla, mlipuko huu unahitaji ushirikiano sio tu kati ya nchi na nchi lakini katika ngazi zote, kwa kuzingatia maelewano ya msaada, ushirikiano, uwazi, kubadilishana rasilimali na katika maeneo yaliyoathirika, kwenda kwa watu walioko kwenye mazingira magumu na wale wanaowajali wengine.​