Nicole Niyoyankunze, an MSF health promotion worker, raises awareness among carpenters in the Bwiza district, Bujumbura. [ Evrard Ngendakumana ]
Access to Healthcare

Bujumbura, wahanga wa ajali watoka wakiwa huru

Ni mapema asubuhi ya mwezi Agosti katika hospitali ya Bwiza-Jabe, mjini Bujumbura, mji mkuu. Kijana fundi seremala mwenye umri wa miaka 20 kutoka Bwiza anawasili akiwa na jeraha la kichwa lililotokana na jiwe lenye ncha kali. Muuguzi anampa huduma ya kwanza, akisimamiwa na Alain Muluvia, muuguzi wa shirika la Madaktari Wasio na Mipaka, MSF.

“Mgonjwa huyu aligongwa na jiwe lililoruka kutokana na kukanyagwa na gari iliyokuwa kasi,” anasema Alain. “Tumempa huduma ya kwanza, lakini ana hitaji kushonwa ndani na nje. Hasa kutokana na jeraha lenyewe, tutamuhamishia L'Arche de Kigobe.”

Wagonjwa 2,000 kwa mwezi

L'Arche de Kigobe ni kituo cha afya kilichoanzishwa na MSF wakati wa vurugu za mwaka 2015 nchini Burundi ili kutibu watu waliojeruhiwa wakati wa vurugu. Mwaka uliofuatia, wakati vurugu zikiwa zimepungua, MSF iliamua kuwatibu watu waliojeruhiwa kutokana na ajali, ambapo idadi imeongezeka kutoka watu 200 kwa mwezi hadi kufikia watu 2,000 kwa mwezi. Hivi sasa kituo hiki kinatoa huduma kwa wahanga wa ajali za barabarani pamoja na majeraha ya moto na wahanga wa vitendo vya ukatili wa kingono.


Surgery at “L’Arche de Kigobe” trauma center . In 2018, we conducted over 4000 surgeries - that's almost 11 a day.  [ ©  Evrard Ngendakumana ] 

“Wagonjwa wetu wanatoka maeneo yote ya nchi,” anasema mratibu wa miradi ya MSF Vincent Onclinx. “Kwa sasa asilimia 90 ni wahanga wa ajali, hasa za barabarani. Mwaka uliopita tulifanya huduma za dharura 22,400 na kufanya upasuaji kwa wagonjwa 4,000, hii ikiwa na maana kuwa ni 11 kwa siku.”

Huku watu wengi zaidi na zaidi wakihitaji msaada, mwezi Juni mwaka 2019 MSF iliamua kujikita katika kutibu wale ambao wanamajeraha ya mateso, ikiwapeleka wale wenye majeraha madogo katika hospitali washirika za jirani kama ya Kamenge na Bwiza-Jabe na vituo viwili vya afya kule Buterere II na Ngagara. MSF inalipia huduma hizi huku ikitoa mafunzo kwa wafanyakazi na misaada mingine.

Kuondoa Vikwazo vya Kifedha

Katika eneo la Bwiza manispaa ya Bujumbura, mhamasishaji wa MSF Nicole Niyoyankunze amesimama mbele ya idadi kubwa ya watu, akiwa ameshika kipasa sauti mkononi. Watu wengi ambao wanaishi na kufanya kazi hapa ni maseremala, kazi ambayo kuumia ni jambo la kawaida. Nicole anafanya vipindi kadhaa vya kutoa taarifa, akiwaambia watu nini cha kufanya pale wanapoumia na wapi pa kwenda kupata matibabu ya bure.

“Katika kituo chetu tunatoa huduma kwa wagonjwa na hawatatakiwa kulipa chochote kupata matibabu,” anasema Nicole. “Hii ni faida nzuri kwa sababu gharama zinaweza kuwa kikwazo kikubwa cha kupata matibabu.”


 Aboul Karim  recovering in one of the wards after an accident in Bujumbura. [ ©  Evrard Ngendakumana ] 

Mvuvi Abdoul Karim aligongwa na gari wakati alipkuwa akivuka barabara. Aliletwa L’Arche de Kigobe, madaktari walimfanyia upasuaji mkono wake. Wiki mbili baadae anaendelea kupata nafuu akiwa wodini.

"Nilipoamka nikiwa katika kituo cha L'Arche siku hiyo, nilikuwa sifahamu mahali nilipo au nimefikaje hapa,” anasema Karim. “Basi nikaanza kukumbuka kipi kilinitokea: nakumbuka gari lilinigonga wakati nikivuka barabara kwenda kuuza samaki wangu.”

Kumbukumbu za Abdoul Karim kuhusu ajali hii huenda zikawa chache, lakini anajua kwa hakika kuwa bila ya matibabu bure, asingeweza kumudu gharama za upasuaji kutibu mkono wake. “Nilipata bahati sana kuletwa hapa,” anasema. “Madaktari walinipasua na kunitibu kama vile ambavyo ningewapa hela. Mimi ni mvuvi tu, napata wapi pesa ya kulipia matibabu haya?”


An MSF physiotherapist L’Arche de Kigobe gives rehabilitation exercises to a young patient whose arm plaster has just been removed.[ © Evrard Ngendakumana]

Kituo cha afya cha L’Arche de Kigobe kina jumla ya vitanda 68 na mara zote vimejaa, kikiwa na wafanyakazi 240 raia wa Burundi na 12 raia wa kigeni na mara zote wana kazi. Pamoja na kutoa huduma za dharura za upasuaji  na mishipa, MSF pia inatoa huduma za mazoezi ya viungo na kisaikolojia ili kuwasaidia kukabiliana na majeraha, kimwili na kiakili, ili wanapoondoka hospitali wawe na ujuzi wa kuendelea na maisha yao.

Kelele za vicheko na upigaji makofi zinasikika katika veranda kuu za kituo. Katika chumba cha utoaji elimu, Amina, msichana mwenye umri wa miaka 7, anaanza mazoezi yake ya kwanza ya viungo baada ya kutumia muda wa mwezi mmoja akiwa na bandeji kutokana na kuvunjika mguu mara mbili. Baba yake anatazama, akifurahi kuona mtoto wake akianza kujifunza kutembea tena.