Outside view of the Barsalogho IDP camp, January 2019 ©MSF/Caroline Frechard
Access to Healthcare

Burkina Faso: Uhitaji mkubwa wa misaada ya kibinadamu kwa nchi

Hali tete ya misaada ya kibinadamu na machafuko ni ya kiwango gani nchini Burkina Faso?

Shambulio la kwanza ambalo makundi ya kijihadi yalikiri kuhusika nalo nchini Burkina Faso lilitekelezwa mwaka 2015. Kuzorota pakubwa kwa hali ya usalama katika kipindi cha miaka miwili iliyopita imeitumbukiza nchi hiyo katika mzozo mkubwa zaidi.

Katika maeneo yaliyoathirika pakubwa na machafuko, mfano, Nord, centre-nord na mikoa ya Sahel, ni vigumu sana kwa siku kupita bila kushuhudiwa machafuko. Zaidi mapigano ya makundi yanayohasimianaa jeshi la serikali na washirika wake, raia wanajikuta katika hali tete ya kuporwa mali zao, kuuawa na mauaji ya halaiki. Mfano wa hivi karibuni ni shambulio katika vijiji kadhaa kwenye mkoa wa Nord jimboni Yatenga, machi 8, kipindi ambacho kwa mujibu wa serikali watu 43 waliuawa. Wahanga wengi walikuwa ni kutoka jamii ya Fulani ambao wamekuwa wakilengwa na jamii nyingine, ama kwa kutuhumiwa kushirikiana na makundi ya kijihadi. Wafanyakazi wetu ambao wameshiriki kuwatibu manusura wa matukio ya hivi karibuni katika hospitali ya Ouahigouya, kuwasikiliza na kuwapa ushauri na kusambaza maji kwa maelfu ya watu ambao wameomba hifadhi katika jimbo la Yatenga.

Ongezeko la idad ya watu ambao wamelazimika kukimbia nyumba zao ni ishara ya hali mbaya ambayo inaathiri jamii mbalimbali nchi nzima. Mwishoni mwa mwaka 2018, karibu watu 48,000 walikosa makazi. Mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka 2019, walikuwa ni 560,000 na leo hii idadi imeongezeka kufikia 780,000. Baadhi ya tabiri zinaonesha kuwa katika kipindi cha miezi michache ijayo kutakuwa na watu zaidi ya milioni moja ambao hawana makazi nchini humo. 

msf308124_medium.jpg

Je msaada unaotolewa na MSF na mashirika mengine inatosha kukidhi mahitaji ya msingi ya watu walioathiriwa na hali inayoshuhudiwa? Tunafanya nini katika mazingira haya?

Kasi ya mizozo inayoshuhudiwa sio tu inaathiri wananchi lakini hata kwa mashirika ya misaada yaliyoko huko, na ni wazi kuwa misaada haitoshi. Idadi kubwa ya watu wasio na makazi inaathiri pia miundombinu kwenye miji ambayo wameomba hifadhi. Kwa mfano, mji wa Titao hakuna tena maji. Timu ya wafanyakazi wetu wamekuwa wakichimba visima kusambaza maji kwa wakazi karibu 10,000 na wale wasio na makazi 20,000 tangu mwezi Novemba 2019, hata hivyo hakikisho la kupata lita 5 za maji kwa mtu mmoja halipo. Timu yetu pia iligawa vifaa muhimu 3,600 kwenye mji wa Titao na Ouindigui. Mamlaka pamoja na shirika la mpango wa shakula duniani WFP wameanza kusambaza chakula, lakini hadi sasa msaada huu umefikia sehemu tu ya watu walioathirika na kuwa na chakula kichache tu ambacho hakiwezi kupunguza lishe bora.

Mfumo wa huduma za afya mara zote uko katika hali mbaya, na vituo vingi vya matibabu kwenye eneo la Sahel, na mkoa wa Centre-Nord, vimefungwa ama havina uwezo kabisa wa kutoa huduma. Tunatoa huduma wa matibabu kwenye maeneo kama ya Barsaloghom Djibo, Ouahigouya, Titao na Ouindigui, lakini kwa sababu za usalama, kufanya shughuli zetu kuna wakati inakuwa ni changamoto. Tunafanya kazi na watu wachache, na baadhi wanalazimika kukaa sehemu moja kwakuwa hawawezi kwenda popote. Maeneo mengine ni rahisi kuyafikia – kama Boucle du Mouhoun, kwa mfano, ambako tunapanga kufanya kampeni ya chanjo ya surua kwa watoto 120,000, wilayani Dedougou na Boromo. Hata hivyo, wakati wowote ule hali huenda ikawa mbaya zaidi.

Mwisho, wengi miongoni mwa watu wanakabiliwa na machafuko. Wanaishi katika maeneo ambayo kuna shughuli kubwa wa kijeshi ambako kamwe hatuwezi kufika. Hatuna hata hakikisho la kawaida tu kuhusu usalama wetu, lazima twende tufanye tathmini ya mahitaji na kutengeneza mkakati mahsusi. Bahn na Sole Kaskazini mwa Titao jirani na mpaka wa Mali ni maeneo tunayoyaangazia hapa.

Hali tete ya misaada ya kibinadamu tayari inaogopesha, na kuna uwezekano mkubwa ikawa mbaya zaidi wakati msimu wa magonjwa ya malaria na njaa vinapoanwa mwezi Juni. Janga kubwa kabisa, lakini je linawuilika? 

Malaria test in the triage room at the advanced health post in Barsalogho, Mali © Noelie Sawadogo /MSF
Malaria test in the triage room at the advanced health post in Barsalogho, Mali © Noelie Sawadogo /MSF

Tunaweka mpango wa kuzuia kama kipaumbele chetu. Ndio, lazima tujidhatiti kuwa tunakuwepo, kutengeneza mtandao na kuwa karibu na jamii ili kuhakikisha tunafika katika maeneo zaidi na kutoa msaada wa kile kinachohitajika. Lakini mamia kwa maelfu ya watu vijijini, mijini na kwenye makambi wanaweza kufikiwa hivi sasa. Kudhibiti usalama ni suala gumu, lakini bado inawezekana kupeleka misaada ya kibinadamu kwenye maeneo kama hayo.

Kipindi cha kati ya mwezi Juni na Octoba mara nyingi ni wakati mtambuka kwa watoto wadogo katika eneo la ukanda wa Sahel. Ni vigumu sana kufanya kampeni ya kusambaza dawa (inaitwa mpango wa kuzuia malari) kawaida hutekelezwa nchini Burkina Faso ili kuzuia mlipuko wa kesi za wagonjwa wa malaria kama kawaida. Hatupaswi kusahau kuwa wengi kati ya watuj 780,000 ambao hawana makazi walilazimika kuacha kila kitu nyuma – ardhi yao, mifugo na rasilimali – na wanataabika na hali mbaya ya kiuchumi ambayo itafanya iwe vigumu kwao kufidia ombwe la njaa lililoko mbele yao. Machafuko yameathiri sekta ya kilimo na biashara imeathirika pakubwa. Wenyeji ambao wanawapa hifadhi watu wasio na makazi nao wako katika shinikizo kubwa.

Kwa hiyo kuna nafasi ndogo tu ya miezi michache ya kusambaza misaada ya dharura kwa kiwango kikubwa na kuepuka msimu wa vifo kama inavyotarajiwa kuanza mwezi Juni. Hii inamaanisha kutoa maji safi na salama, usambazaji wa chakula na virutubisho na kuhakikisha upatikanaji wa huduma za afya. Muda bado haujaisha. Juhudi za misaada, na hii ikijumuisha msaada wa MSF, lazima iongezwe kwa haraka sana.

Kifo cha kwanza cha mgonjwa wa Corona katika eneo la Jangwa la Sahara kinaripotiwa nchini Burkina Faso. Je ni kitu kingine kikubwa cha kuhofia?

Kisa cha kwanza kiliripotiwa mjini Ouagadougou Machi 9, mtu ambaye alipata maambukizi ya COVID-19 akiwa Ufaransa na kisha watu wengine walifuata – walifikia 28 hadi kufika Machi 18. Hii inaogopesha sana hasa kwa nchi ambayo tayari inakabiliwa na hali tete kibinadamu na matokeo yake sekta ya afya kudhoofishwa.

Timu iko katika mawasiliano na mamlaka za nchi hiyo kufanya tathmini ya namna ya kusaidia wakati huu wa mlipuko wa COVID-19, kuwabaini wagonjwa na kudhibiti maambukizi. Katika aina hii ya milipuko, wafanyakazi wa afya wanakuwa mstari wa mbele. Ni muhimu sana kuhakikisha wanalindwa dhidi ya hatari ya COVID-19 na kupata msaada hitajika wa matibabu watakapohitaji.

Makataa ya kusafiri na hatua nyingine zilizochukuliwa kuzuia muingiliano wa watu pia ni changamoto kwetu. Inaweza kutuzuia kutuma wafanyakazi wetu ambao ni wazoefu nchini Burkina Faso, ambapo uwepo unahitajika kusaidia kupunguza makali ya hali mbaya ya kibinadamu katika majuma kadhaa yajayo.