Esther anajaribu kufumbua macho kidogo wakati madaktari wa walipomchoma chanjo ya majaribio iliyofanyiwa utafiti, ikifahamika kama rVSV-ZEBOV kwenye mkono wake wa kushoto mjini Kimbangu, eneo lililoko kusini magharibi mwa mji wa Beni. Justin, akiwa na mtoto wake mwenye umri wa miaka miwili na nusu, anaangua kilio pale anapoona sindano ikijazwa dawa na anatulia dakika chache baada ya kuchomwa. Chanjo hii inauma kidogo kwenye mkono, lakini madhara ya baadaye ni kidogo na matokeo yanaonesha chanjo hii imekuwa na ufanisi wa kukinga kwa zaidi ya asilimia 95 baada ya mtu kuchomwa ndani ya siku 10.
MSF inaongoza timu tatu zinazotoa chanjo mjini Beni, kila timu ina watu 14 kwaajili ya kusajili watu kwa chanjo, kuhakikisha utayari wao, kukusanya taarifa, kuchoma chanjo na kuwatazama waliochanjwa kwa dakika 30. [ © Picha: MSF/ Samuel Sieber ]
Esther na mtoto wake wa kiume walikuja katika moja ya vituo vitatu vilivyoanzishwa na MSF kila siku mjini Beni, kama sehemu ya juhudi za kudhibiti Ebola kwa pamoja kwa kushirikiana na wafanyakazi kutoka wizara ya afya na shirika la afya duniani. “Kulikuwa na mtu ambaye ni jirani yangu aliyethibitishwa kuwa na Ebola na timu ya ufuatiliaji iliniambia tunapaswa kwenda kupata chanjo kutokana na uwezekano kuwa huenda tulikutana nae”, alisema Esther.
Kutengeneza sehemu ya kutoa chanjo ni jambo ambalo hupangiliwa vizuri sana. Kuna meza za plastiki na zimepangwa katika eneo la kusubiri, fomu ya usajili na ile ya kukubali zimewekwa mezani na timu ya kutoa chanjo wanavaa nguo za kujikinga. Halafu gari la MSF linawasili likiwa na makasha maalumu yenye chanjo, na mmoja wa watu walio katika timu ya ufuatiliaji anaanza kuwabaini wanaostahili kuchanjwa.
Wakati huu kesi za Ebola zikiwa zimepungua kwenye mji wa Beni tangu mwishoni mwa mwezi Agosti 2019, bado kuna kesi mpya na kesi zilizothibitishwa na kufikishwa katika vituo vilivyotengwa na wizara ya afya au katika vituo ambavyo vinasimamiwa na MSF kila siku. Kwa zaidi ya mara mbili sasa, Mwezi Desemba 2018 na Juni 2019, mlipuko wa Ebola unaonekana kudhibitiwa, lakini unarudi tena kwenye baadhi ya maeneo tena kwa idadi kubwa.
Wakati chanjo ikionesha ufanisi, kuweka ukomo wa upatakanaji wake kunawalenga wale waliokutana au ambao hawajakutana na watu wenye Ebola. Ni asilimia 25 pekee kwa sasa ya watu wanaweza kufikiwa. [Picha na: MSF/ Samuel Sieber ]
Ebola imebakia kuwa ugonjwa hatari. Licha ya uwepo wa chanjo kuzuia maambukizi na matibabu mapya kwa kesi zilizothibitishwa, zaidi ya watu 3,100 wameambukizwa tangu kuripotiwa kwa mlipuko huu wa 10 na mkubwa zaidi nchini DRC, na zaidi ya watu 2,100 wamekufa mpaka kufikia katikati ya mwezi Septemba. Wagonjwa wakionesha dalili za homa, kuharisha au kutapika wanapaswa kutengwa na kutibiwa haraka iwezekanavyo. Hata hivyo Kivu Kaskazini yote muda wa kugundua kesi ya dalili za ugonjwa wa Ebola ni siku tano, ambapo wakati huu wengi huwa wanasafiri na kutembelea vituo vya afya.
Kuwatambua na kutoa chanjo kwa watu waliokutana na wagonjwa kama Esther na Justin ni muhimu kuwalinda watu walioko hatarini, na ni suala ambalo ni moja ya changamoto kubwa katika vita ya kudhibiti mlipuko huu. Timu tatu za MSF zimesaidia kutoa chanjo zaidi ya 700 katika majuma mawili ya mwanzo pekee, na watu zaidi ya 51,000 wamepewa chanjo kwenye mji wa Beni na timu ya kitaifa ya kukabiliana na Ebola kwa kushirikiana na washirika.
Hata hivyo kutokana na uwepo wa ukomo wa matumizi na hali ya utafiti wa chanjo yenyewe, mkakati wa utoaji chanjo jimboni Kivu Kaskazini, kwa sasa umewekewa mpango maalumu. Ni watu waliokutana aua kuhisiwa kukutana na kesi za Ebola zilizothibitishwa au wafanyakazi walioko mstari wa mbele kama vile madaktari na wafanyakazi wa misaada, ndio wanalengwa na kampeni hii ya sasa. Tangu kutokea kwa mlipuko, timu ya kitaifa ya ufuatiliaji imefanikiwa tu kudhibiti robo ya kesi zinazofahamika na watu wanaohisiwa kukutana na mtu aliyeambukizwa, huku wengi wakiwa hawajabainika au hata kufuatiliwa kabisa. MSF inatoa wito wa kuundwa kwa kamati ya kimataifa na huru ili kufanya tathmini na kupanua wigo wa mpango uliopo na kuhusishwa na usambazaji wa chanjo kwa uwazi.
“Tunapenda kuongeza wigo wetu wa mkakati wa kutoa chanjo na kuwa huru katika kufikia kanda za afya ambazo zina wagonjwa waliothibitishwa, lakini kwa mpango wa sasa ambao una ukomo wa kutoa chanjo yenyewe kulingana na idadina kufanya kazi katika vituo vya awali vya chanjo”, alisema Joseph Musakane, mratibu wa shughuli za MSF.
Joseph MbokaniI Kambale, muhamsishaji kutoka timu ya kitaifa inayokabiliana na Ebola, akijibu maswali kutoka kwa watu waliokuwa wanasubiri kupewa chanjo. Hofu na uelewa mbaya kunawafanya watu wengi zaidi wanaostahili kupewa chanjo kutojitokeza. [Picha :MSF/Samuel Sieber]
Hofu inayoendelea na uelewa mbaya kuhusu chanjo miongoni mwa jamii, kunaongeza changamoto zaidi kwa timu zinazotoa chanjo. “Wengi wanaamini chanjo inasababisha madhara ya uzazi, magonjwa ya akili au hata Ebola yenyewe, alisema Joseph Mbokani Kambale, muhamasishaji kutoka timu ya kitaifa ya kukabiliana na Ebola. “Makosa mengine ni kufanisha Ebola sawa na magonjwa mengine au kupewa sumu na mara nyingi tunahitajika kuwashawishi watu waje na kupewa chanjo”, aliongeza.
Katika mkutano wa jukwaa la vijana mjini Beni, Meneja mradi wa MSF Jean Pierre Kaposo anafafanua kuhusu kampeni ya chanjo ya Ebola kwa vijana na viongozi wa kijadi. [Picha: MSF/Samuel Sieber ]
Kufanya chanjo iwe inapatikana kwa urahisi zaidi na kujenga imani na jamii, imethibitisha kuwa muhimu kwa wagonjwa ambao wanaonesha dalili za Ebola mwanzo tu wakati wa mlipuko wenyewe. Mwanzoni, MSF ilikuwa ikifanya kazi katika vituo vikubwa vilivyokuwa vinatibu watu wanaohisiwa kuwa na Ebola, lakini punde tuligundua kuwa njia nzuri ni kuwaweka wagonjwa jirani zaidi na jamii zao kwa kuwatengea eneo maalumu. “Tukaanza kutengeneza vituo maalumu vidogo katika vituo sita vya afya mjini Beni, ambako wagonjwa na wale wanaohisiwa walihisi kuwa huru zaidi”, alisema Tristan Le Lonquer, mratibu wa masuala ya dharura wa MSF mjini Goma.
Katika kituo hiki cha afya cha Kanzulinzuli, MSF inatoa chanjo kwa watu waliokutana na mgonjwa na wafanyakazi walio mstari wa mbele. Jengo hili pia lina sehemu maalumu na sehemu ya matibabu kwa kesi zinazodhaniwa kuwa ni maambukizi ya Ebola, na zaidi MSF inasaidia huduma nyingine na zile za maabara. [Picha: MSF/Samuel Sieber]
Vituo hivi vya afya sasa hata vinatoa uwezekano wa kuwa na eneo la kutoa chanjo, ikitoa usalama na uhuru kwa jamii. Wakati huohuo, MSF inaimarisha mifumo ya awali iliyopo katika kutoa huduma za afya. “Tunasaidia kutoa huduma kwa wagonjwa wanaohamishika, uzazi au maabara, ambayo inahitajika sana na iko hatarini kusahaulika wakati wa kukabiliana na Ebola”, aliongeza Le Lenquer.
Chanjo ya pili ya majaribio inahitaji dozi mbili kutolewa katika siku 56 ambapo imeshapewa kibali cha kutumika nchini DRC kama sehemu ya kuongeza wigo wa matibabu ya majaribio, na MSF na timu yake ya utafiti inashiriki kama viongozi wa kidunia katika kuisambaza.
Rekodi za wagonjwa katika kituo kinachosaidiwa na MSF mjini Boikene. Wakati wa kukabiliana na Ebola, vituo vya dharura vya afya viko hatarini kusahaulika. [Picha: Samuel Sieber/MSF]
Mjini Beni, kumaliza maambukizi ya Ebola bado ni suala mtambuka na kazi ngumu, na ni hivi karibuni MSF imechukua kituo kikubwa zaidi cha matibabu ya Ebola ambacho kina vyumba 13 vilivyotengwa kwa huduma za dharura, wodi 3 kubwa zilizotengwa zinauwezo wa kuhudumia wagonjwa hadi 40 na kuna wafanyakazi zaidi ya 160.
“Ili kuvunja mnyororo wa maambukizi, inatuhitaji kuongeza mkakati wa utoaji chanjo, kuweka mpango shirikishi na machaguo ya tiba, kuwa na kituo cha ETC, lakini pia kuendeleza mahitaji mengine ya afya na kujenga uhusiano wa kuaminiana na jamii. Tunahitaji kuwepo katika maeneo yote ili kushinda vita ngumu ya Ebola”, alimaliza kusema Le Lonquer.
* Majina ya washiriki yamebadilishwa kuwalinda.