Hospital installation by MSF in Leganes, Spain © Olmo Calvo /MSF
Access to Healthcare

COVID-19: MSF yaongeza kasi ya kusaidia barani Ulaya

Ili kusaidia kukabiliana na COVID-19 barani Ulaya, shirika la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) limetanua huduma zake nchini Italia, Hispania, Uswis, Ufaransa, Norway, Ugiriki na Ubelgiji.

Akielezea namna MSF inavyoshughulikia janga la COVID-19 barani Ulaya, Dr Christos Christou, rais wa MSF anasema: :

Kama shirika la misaada ya dharura, Msf inatoa misaada ya matibabu kwa watu walio katika mazingira magumu wakati wa majanga na hali mbaya ya kijamii. Hivi leo Ulaya, moja ya maeneo yeney miundombinu bora kabisa ya afya duniani, inatikiswa na shinikizo la ugonjwa wa COVID-19. Kushughulikia masuala ya milipuko ni moja ya nguzo kuu ya kazi tunazofanya – kuingilia kati pale mfumo unapozidiwa uwezo na pale tunapoweza kutoa ujuzi wetu katika kushughulikia mambo ya dharura kwa matumizi mazuri.

 

Shughuli za MSF barani Ulaya

KUWASAIDIA WAZEE

MSF in the nursing homes for the elders to protect guests and staff in Marche region.
Timu ya MSF ikitoa mafunzo  kwa wafanyikazi katika nyumba za wazee katika mkoa wa​ Marche , Italy

Wazee ni miongoni mwa makundi ambayo yameathiriwa pakubwa na mlipuko wa COVID-19. Nchini Italia, Ubelgiji na Hispania, MSF imepanua wigo wa shughuli zake kwa kutoa huduma katika makao ya wazee. Watu wanaoishi kwenye makao haya mara nyingi hugusana na watu, na makazi haya mara nyingi hayana vifaa maalumu.

Kwenye mkoa wa Marche nchini Italia, madaktari wa MSF, wauguzi na wataalamu wa usafi wanawasaidia wafanyakazi wa manispaa kutengeneza itifaki wa kuzuia na udhibiti. Nchini Hispania, MSF inatoa ushauri kwa makazi ya wazee kuhusu njia za kuzuia, kufanya tahmini ya hatari na utekelezaji wake. Nchini Ubelgiji, MSF inatoa huduma ya uelimishaji kuhusu afya na njia za kujikinga katika makazi ya kulea wazee ndani na nje ya jiji la Brussels.

 KUWASAIDIA WAHAMIAJI, WAKIMBIZI NA WASIO NA MAKAZI MAALUMU

Bastien Mollo, MSF doctor, is examining people evacuated from a camp near Paris on March 24th. © Agnes Varraine-Leca/MSF
Bastien Mollo, daktari MSF , akichunguza watu waliohamishwa kutoka kambi karibu na Paris​ tarehe Machi 24 ©Agnes Varraine-Leca/MSF

Nchini Ubelgiji, Ufaransa na Uswis, MSF inawasadia watu ambao wanaishi katika mazingira magumu, kama vile wasio na makazi au wahamiaji. Watu wanaoishi kwenye maeneo yenye msongamano mkubwa, mitaani, katika mahema ya muda au kwenye maeneo ya makazi ambayo ni hatarishi. Wengi tayari afya zao zimezorota, mara nyingi ni kutokana na maisha wanayoishi. Virusi huishi katika maeneo ambayo hayana maji na sio masafi. Na zaidi, watu walio katika mazingira haya hawajumuishwi katika mifumo ya afya.

Jijini Brussels, MSF imetenga vitanda 50, na ina uwezo wa kuongeza hadi kufikia vitanda 150. Vituo hivi vinatoa nafasi ambayo wahamiaji na wale wasio na makazi maalumu kutengwa, kupokea matibabu na kupelekwa hospitali.

Jijini Paris na mazingira yanayozunguka, MSF inaingilia kati kusaidia watu walio katika mahema ya dharura, ikisaidia kuwabaini wale ambao tayari wana maambukizi ya COVID-19, katika siku zijazo, timu yetu inalenga kupanua wigo wa huduma ili kuwasikiliza watu wanaoishi mitaani. Mjini Geneva, MSF inatoa msaada wa ugavi na kusaidia mifumo ya afya kwa ajili ya watu wanaoishi katika mazingira magumu, na pia kuwafundisha wafanyakazi na wanaojitolea na kufanya kazi na haya makundi.

 KUZISAIDIA HOSPITALI NA KUWAWEKA WAFANYAKAZI WA AFYA SALAMA

Hospital installed by Medicos Sin Fronteras to treat coronavirus patients in Alcala de Henares. © Olmo Calvo / MSF
Hospitali iliyo ezekwa na MSF  kutibu wagonjwa wa virusi vya corona  Alcala de Henares, Hispania. © Olmo Calvo / MSF

Nchini Hispania, MSF imetengeneza vituo viwili vyenye uwezo wa kubeba vitanda zaidi ya 200 ili kusaidia hospitali za Madrid. Kikosi kazi kinasaidia vitengo vya dharura vya hospitali kwa kuwachukua wagonjwa wa kawaida, ili chumba cha wagonjwa mahututi na vile vya dharura vijikite katika kuhudumia watu wanaougua zaidi COVID0-19. Vikisimamiwa na madaktari wa hospitali, MSF inatoa msaada wa kuratibu na ufuatiliaji. MSF pia inatoa ushauri kwa mamlaka za afya kutengeneza vituo vya muda ili kupanua uwezo wa hospitali zilizopo mjini Madrid, Catalonia – ikiwemo hospitali mbili mjini Barcelona na Vitoria.

Nchini Ubelgiji, MSF inasaidia hospitali 5 kwenye miji ya Hainaut na Antwerp, ikitoa ushauri wa kiufundi na mafunzo na iko tayari kuongeza uwezo wa kupokea wagonjwa.

Nchini Uswis, MSF inasaidia hospitali ya chuo kikuu cha Geneva, ikitoa ujuzi kusaidia namna bora ya kuhudumia wagonjwa ambao wamepata maambukizi ya COVID0-19, na kwa kushirikiana na wataalamu wa afya na watoa huduma wengine katika hospitali. Chini ya uratibu wa hospitali ya chuo kikuu cha Geneva, MSF ina kituo kinachotembea na kiko tayari kutoa huduma ya nyumbani kwa wagonjwa wa COVID-19, ambao hawana vigezo vya kupelekwa hospitali. Kwa kushirikiana na mji wa Geneva, MSF imetoa mapendekezo kwa uma na sehemu binafsi za kuhifadhia maiti kuhusu utaratibu wa kuepuka kupata maambukizi wakati wa kufanyia mwili uchunguzi.

MSF pia inatoa msaada wa ushauri kuhusu mikakati na utekelezaji wa itifaki wa kujikinga kwa hospitali zilizo jirani na mji wa Oslo nchini Norway, katika moja ya maeneo ambayo ni kitovu cha kesi za wagonjwa nchini humo. Nchini Ugiriki, timu yetu inatoa msaada katika kambi zilizotelekezwa za visiwa vya Samoa na kufanya tathmini ya mahitaji ya hospitali. Katika kisiwa cha Lesbos, MSF imeandaa mpango wa dharura kwa wajili ya kambi ya wakimbizi ya Moria, ikiwa tu mlipuko huu utaendelea.

Maeneo zaidi
February 2020: An MSF health promotion session in Hong Kong   © Shuk Lim Cheung/MSF

Timu ya MSF pia inasaidia shughuli za COVID-19 kwa kushirikiana na mamlaka za afya kutoka Afghanistan hadi Libya, Nigeria hadi Syria na hata Hong Kong.

MSF imeshuhudia namna ambavyo mlipuko wa ugonjwa huu umeharibu mifumo ya afya ya nchi zilizoendelea, katika nchi ambazo zina usalama wa kijamii ambako watu karibu wote wana uwezo wa kupata maji safi na salama na maeneo ya kujitenga. Hii sio rahisi kabisa kwa watu wa nchi ambazo tunafanya kazi. Hofu yetu kubwa ni ikiwa virusi hivi vitasalia katika nchi yenye mfumo duni wa afya na kwenye watu ambao hawana uwezo wa kujilinda. Ushirikiano wa kimataifa utakuwa muhimu sana, huku namna ya kushughulikia COVID-19 ikitengenezwa kwa kuzingatia mazingira tofauti, jamii na kuwajengea uwezo watu.

“Leo, ngazi zote za MSF zimeguswa, na kuleta changamoto, na kuhitaji ushirikiano zaidi na ubunifu wa kupata suluhu. Tunajaribu kuzoea haraka iwezekanvyo ili kuwa na uwezo wa kukabiliana na COVID-19 katika miradi yetu duniani, licha ya makataa ya kusafiri na uhaba wa upatikanaji wa vifaa,” anamaliza Dr Christos. Kila mahali tuliko duniani tunafanya kazi ili kuendelea shughuli zetu za kutoa msaada wa kiafya wakati huu kukiwa na ongezeko kubwa la changamoto za kusafiri na mbinyo wa kusambaza biadhaa.