New Ebola Vaccine [Photo: Gabriella Bianchi/MSF]
Access to Healthcare

Ebola DRC: “Tuna imani kuwa chanjo hii itatupa uchaguzi zaidi wa mustakabali wa milipuko ya baadae”

Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka ni washirika wa mashirika mengine ya kimataifa ambayo yalihusika na utafiti huu, na itasimamia utekelezaji wake kwa kushirikiana na wizara ya afya na taasiri ya utafiti ya magonjwa ya mlipuko.

Timu ya MSF imekuwa ikikutana na wanajamii kwenye mji wa Majengo na Kahembe kwenye wilaya za Goma, ili kubadilishana taarifa kuhusu chanjo na kujibu maswali yao. Wilaya hizi mbili zimebainishwa kwa kushirikiana na maofisa wa afya kuwa maeneo ya kwanza yatakayopata chanjo.

Timu ya kinga iliyopewa mafunzo ndio itaanza kutoa chanjo hii kwenye vituo hivi viwili, huku vinne zaidi vikitarajiwa kubainishwa katika majuma kadhaa yajayo. Itatolewa kwa watu wazima na watoto wenye umri wa mwaka mmoja na zaidi kwa mujibu wa maelekezo ya utafiti, na tunalenga watu 50,000 katika kipindi cha miezi minne.

John Johnson, kiongozi wa miradi wa MSF kwaajili ya chanjo hii na karibuni alikuwa mjini Goma kusaidia kuzindua.

Kwanini tunahitaji kuzindua chanjo ya pili ya Ebola?

Chanjo ni moja ya kifaa muhimu kinachowalinda watu dhidi ya virusi vya Ebola. Chanjo ya  Merc’s rVSV ZEBOV imeonesha kuwa na ufanisi mkubwa na imekuwa chanzo muhimu katika vita dhidi ya mlipuko wa Ebola. Kuzinduliwa kwa chanjo ya pili haimaanishi ni kuchukua nafasi ya chanjo ya rVSV, lakini ni kuongeza wigo na tuna imani itatuongezea nyenzo katika vita dhidi ya milipuko mingine ya Ebola. Huu ukiwa ni mlipuko wa 10 wa Ebola nchini DRC, inaonesha ni jinsi gani ilivyo muhimu kuwa na chanjo nyingine kutolewa nchini humo.

msf293005_medium.jpg

Ni malengo gani hasa ya kutambulisha chanjo hii ya pili?

Lengo la awali la utafiti huu ni kupata taarifa kuhusu ufanisi wa chanjo katika uhalisia wa dunia ya sasa. Utafiti wa kimaabara unaonesha kuwa chanjo hii inaongeza kinga dhidi ya Ebola, lakini njia pekee ya kuthibitisha ufanisi wake nje ya maabara ni kwa kuitoa chanjo hii wakati wa mlipuko. Kirahisi unaweza kusema, utafiti huu unalenga kuwa chanjo itasaidia kuwalinda watu wakati wa milipuko mingine.

Kuna sababu nyingine za kufanya utafiti wa chanjo hii kidunia. Kwa mfano, kujifunza ni namna gani chanjo itakubaliwa na watu, kutathmini mgawanyo wa dozi zote mbili wakati wa mlipuko, na kuona ikiwa watu watarudi kwaajili ya dozi ya pili. Na licha ya kuwa chanjo ya J&J ina rekodi nzuri ya usalama katika tafiti za awali kwa binadamu, tutaendelea kukusanya taarifa za kuhusu usalama wake. Zaidi, utoaji na kuchunguza chanjo hii kutasaidia uratibu wa matumizi yake wakati wa milipuko mingine.

Kwanini chanjo hasa ilichaguliwa? Unajuaje kuwa ni salama?

Chanjo hii ilithibitishwa kwa mapendekezo ya muda na wataalamu wa SAGE kuhusu kinga yake mwezi Mei mwaka 2019.  ilichaguliwa kwa sababu ilionesha kuwa na ufanisi kati ya chanjo nyingine zilizotafitiwa. Lakini pia ni kwa sababu ilikuwa imevuka hatua ya kwanza na ya pili kimajaribio, ambapo binadamu 6,000 walijitolea kushiriki. Utafiti huu ulionesha kuwa chanjo hii ina wasifu mzuri wa kiusalama.

Ni kwa namna gani kupungua kwa idadi ya kesi mpya za Ebola kunaathiri utafiti huu?

Kuripotiwa kila siku kupungua kwa kesi mpya za maambukizi ya Ebola ni habari njema, hata hivyo itafanya kuwa vigumu kuthibitisha ufanisi wa chanjo yenyewe. Tunalenga kutoa chanjo hii kwenye maeneo jirani ambayo ugonjwa wa Ebola umeendelea kuenea na tuna imani kuwa itatoa kinga kwa jamii zilizoko hatarini. Ikiwa mlipuko utaendelea na baadae kufika kwenye maeneo ambayo watu wake walipewa chanjo, tutajua wakati huo ikiwa watu waliokuwa wamepewa chanjo wana kinga. Hii itakuwa ushindi kwa raia na ishara kuwa chanjo imekuwa na ufanisi.