msf293174_medium.jpg
Access to Healthcare

MLIPUKO WA KIPINDUPINDU NCHINI BURUNDI: “SHUKRAN ZA DHATI, FAMILIA YANGU IMERUDI IMEPONA”

Tangu mwezi Juni mwaka 2019, nchi ya Burundi imeshuhudia mlipuko mkubwa wa kipindupindu. Zaidi ya kesi 1,000 zimerekodiwa, nyingi ni kutoka mji mkuu wa nchi hiyo Bujumbura.

Ugonjwa huu hatari, kipindupindu kinaambukizwa kutokana na bakteria Vibrio Cholerae – ambao wanatokana na uchafu na maji yaliyotuama. Unasababisha kuhara na kutapika, kipindupindu husababisha kupoteza maji mengi mwilini na bila ya tiba mahsusi unaweza kuua ndani ya saa chache.

“Watoto wangu wawili walianza kuumwa siku ya Jumapili na walianza kuharisha,” anasema Sandrine, mgonjwa katika kituo cha kutibu kipindupindu kinachosimamiwa na MSF mjini Bujumbura. “Kituo cha kwanza cha afya nilichowapeleka walibaini ni kuharisha tu. Lakini hali zao zilizidi kuwa mbaya na mwishowe nikaleta gari la wagonjwa. Siku mbili baadae, mtoto wangu watatu aliungana nao. Sijui wote imetokeaje wakaumwa. Niliumwa pia na mimi nikalazwa hapa.”

Sandrine Ntirampeba

Huduma ya haraka

Ugonjwa huu sugu unaenea kutokea maeneo ya ziwa Tanganyika na mto Rusizi, kipindupindu kinaripotiwa kuwaathiri watu katik ya 200 na 250 kila mwaka nchini Burundi. Lakini kila miaka mitano hadi sita, nchi hiyo inashuhudia ongezeko la visa vya ugonjwa huu. Katika mlipuko wa mwaka 2013, watu 936 waliambukizwa kipindupindu katika majimbo ya Bubanza na Cibitoke na watu 17 walikufa kutokana na maradhi haya.

“Mwaka huu, mlipuko umekuwa wa kasi sana, na umeathiri Bujumbura mji ambao una idadi kubwa ya watu nchini humo,” anasema Julien Binet, mwanasheria wa shirika la Madaktari Wasio na Mipaka nchini Burundi. “Kwa kuzingatia ukubwa wa mlipuko na hatari iliyopo, tumeanza mara moja kufanya kazi na mamlaka za nchi hiyo kusaidia vituo vya matibabu.”

Kwa miaka, MSF imekuwa shirika la misaada la kimataifa ambalo linaisaidia wizara ya afya na mamlaka nyingine katika kuwahudumia wagonjwa wa kipindipindu. Ushirikiano huu wa karibu umejikita katika huduma za matibabu, mafunzo kwa wafanyakazi, kutengeneza kampeni za kueneza uelewa na wakati inapohitajika, vituo vya matibabu ya kipindupindu kulingana na mwaka wenyewe.

“Hata kabla ya tangazo rasmi la mlipuko wenyewe mwezi Juni, timu ya MSF ilikuwa tayari imeanza kusaidia udhibiti wa kesi za kipindupindu zilizotokea mwezi januari kwenye jimbo la Rumonge,” anasena Binet. “Msaada huu umeongezeka zaidi katika kipindi cha miezi kadhaa, shukrani kwa huduma za haraka, kumekuwa hakuna wahanga kabisa nchini, licha ya idadi kubwa ya kesi za wagonjwa. Na idadi ya walioambukizwa pia imepungua, jambo ambalo ni ishara nzuri.”

A young woman with symptoms of cholera sits in the triage room of the MSF-supported new cholera treatment centre in Bujumbura. In the triage room, MSF and public health staff diagnose patients and provide initial care.

Kituo kipya Bujumbura.

Hivi leo, MSF inasaidia vituo vitatu vya matibabu ya kipindupindu nchini Burundi, ikisimamia na kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wa Burundi. MSF inalenga kutoa huduma bure kwa wagonjwa wakati ikiwajengea uwezo wafanyakazi wa afya. Kwa kuwa ugonjwa huu unahusishwa na watu kukosa huduma ya maji safi na salama ya kunywa, MSF imejenga majaba makubwa ya maji mjini Bujumbura ba kwenye majimbo ya Rugombo, Ndava na Cibitoke.

Kituo kipya cha matibabu ya kipindupindu kilifunguliwa mwezi Octoba mjini Bujumbura. Kikitengenezwa na MSF ndani ya wiki mbili, kituo hiki chenye vitanda 50 kwa sasa ndio kituo kikuu cha matibabu, kikichukua nafasi ya kile cha mwanamfalme Regent Charles, ambacho kilishindwa kuwahudumia wahitaji.

“Mtoto wangu wa kike waliwasili katika kituo hiki akiwa dhaifu, masikio yakiuma, kutapika na kuharisha,” anasema Chany, mama wa mtoto wa miaka 3 Shemsu. “Shukrani kwa huduma nzuri iliyotolewa kituoni hapa, ilimchukua siku chache tu kurejea kwenye hali yake ya kawaida.”

Chany Manirakiza and her three-year-old daughter, Shemsu, who was recently treated at the MSF-supported new cholera treatment centre in Bujumbura.  [Evrard Ngendakumana/MSF ]

“Kabla ya kuondoka, tulipewa ushauri wa namna ya kuepuka ugonjwa huu,” anasema Chany. “Nimeuchukua ushauri huu, lakini baadhi ya majirani wanafikiri kuwa kipindupindu hakitawafikia kwa sababu wamezoea uchafu. Wanafikiri wana kinga. Inathibitisha kuwa hawaujui ugonjwa.”

Kueneza uelewa, suala la msingi.

Kueneza uelewa ni suala la msingi katika mapambano ya kuenea kwa mlipuko wa magonjwa. Hata kama upatikanaji wa maji safi na hali ya usafi ikibakia changamoto nchini Burundi, kuna njia rahisi na zente matokeo chanya ambapo watu wanaweza kuzitumia kujilinda dhidi ya maambukizi ya kipindupindu.

A community health worker with a megaphone raises awareness about cholera in Bujumbura’s Buterere market. [ Evrard Ngendakumana/MSF]

Siku moja mchana mwezi Octoba, wafanyakazi wa kijamii wanaosaidiwa na MSF wanasambaza ujumbe wa kujikinga njini Bujumbura kwenye soko la Buterere. Wakiwa wamebeba vipasa sauti, wanawaeleza watu kuhusu umuhimu wa kuosha mikono kabla na baada ya mlo, kupika mboga na kuosha matunda ili kuua bakteria. Pia wanaeleza namna unaweza kutambua dalili za awali za kipindupindu na nini cha kufanya ikiwa watahisi wao au mwanafamilia ameambukizwa.

“Familia yangu yote imepata kipindupindu,” anasema Zacharia, ambaye aliruhusiwa kutoka katika kituo cha matibabu ya kipindupindu kinachosaidiwa na MSF mjini Bujumbura baadaya wiki kadhaa za kuwekewa maji na kutibiwa. “Shukranim kila mtu alirudi amepona. Leo hii, tunajua kwenye familia kuwa kuosha mikono kunaweza kuokoa maisha yetu. Lakini kila mtu anapaswa kujua hili!”