Entrance of MSF hospital in Nduta refugee camp
Access to Healthcare

Wakimbizi na jamii nyingine katika kambi za Tanzania wako hatarini kupata COVID-19 ambako huenda maambukizi yakawa mabaya zaidi

Pete Clausen ni mkurugenzi wa MSF nchini Tanzania
Mimi ni muwakilishi wa shirika la Madaktari Wasio na Mipaka nchini Tanzania, ambako timu yetu inahudumia hospitali yenye vitanda karibu 150 na vituo vinne katika kambi ya wakimbizi ya Nduta, jirani na mpaka na nchi ya Burundi. Kambi ya Nduta ni nyumbani kwa wakimbizi wa Burundi karibu 73,000 ambao walikimbia nchi yao kutokana na machafuko ya mwaka 2015.

Katika kambi ya Nduta, timu yetu ya watu 800 na wengine wanaojitolea wanafanya kazi usiku na mchana, kutibu maelfu ya wakimbizi na jamii jirani kila siku kutokana na Malaria, magonjwa ya mfumo wa hewa na kuharisha, pamoja na wale ambao wana magonjwa yasiyo ya kuambukiza, na matatizo mengine ya kiafya.

Tukiwa watoa huduma pekee wa afya katika kambi ya Nduta, wasiwasi wa MSF katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita ni kwa kiasi gani watu hawa wako hatarini kupata maambukizi ya COVID-19, ni kwa kasi ya kiwango gani maambukizi yataenea katika kambi, na utakuwa na madhara gani kwa wagonjwa wetu wenye magonjwa sugu, kama vile HIV, magonjwa ya ukosefu wa chembe hai nyekundu za damu (sickle cell) na kifua kikuu.

Ikiwa hautadhibitiwa mapema, maambukizi ya COVID-19 kwenye kambi ya Nduta yanaweza kuongezeka kwa kiwango cha juu ndani ya wiki chache na kusababisha idadi kubwa ya vifo. Hii ni kutokana kwa sehemu na hali ya maisha, ambapo watu wanaishi katika makazi ya muda, na kutokuwa na mahitaji ambayo yanasemwa kuwa ni ya kawaida kama vile maji na usafi.

Hali ya watu kujitega binafsi na kuepuka msongamano ambayo jamii nyingine zinauwezo wa kufanya hivyo….haliwezekani katika kambi ya Nduta ambako familia ya watu watano wanaishi katika chumba kimoja. Mazingira duni yanafanya hali ya usafi kuwa ngumu kabisa kufanyika. Tayari Januari mwaka huu, timu yetu imerekodi idadi kubwa ya watu walipata matatizo ya kuhara na maambukizi ya mfumo wa hewa, na kwa sasa tayari hema letu moja limejaa kupita kiasi.

Mlipuko wa COVID-19 katika hali hii inaweza kusababisha kuwa na idadi kubwa ya wagonjwa wenye maambukizi sugu, na kuweka shinikizo kubwa kwa hospitali za MSF na mfumo mzima wa afya katika kambi. Kukiwa na huduma finyu za wagonjwa kutoka nje katika mkoa, maeneo machache ya kutenga watu, na uhaba mkubwa wa vifaa kinga kidunia, mlipuko katika kambi ya Nduta utafanya kuwa vigumu sana kukabili maambukizi haya.

Wakimbizi wa Burundi nchini Tanzania ni miongoni mwa wakimbizi ambao wanabajeti ndogo zaidi duniani, kwa mujibu wa shirika linalohudumia wakimbizi, wakati mkoa wa Kigoma, ambako kambi ya Nduta ipo, ni mikoa masikini zaidi Tanzania. Vivyo hivyo, kwa wakimbizi na jamii zinazozunguka wako hatarini sana kukumbwa na mlipuko. Kuweka hili kwa urahisi, ikiwa mlipuko wa COVID-19 utatokea hapa, maambukizi yatakuwa magumu kuyazuia.

Timu ya MSF kwenye kambi ya Nduta wamekuwa wakiweka mikakati ya kujiandaa kulingana na mazingira, lakini kutokana na uhaba wa vifaa na wafanyakazi, hakuna kile kikubwa tunaweza kufanya. Kwa hivyo, tunatoa wito kwa jamii ya kimataifa kuhakikisha inasaidia nchi ya Tanzania kukabiliana na maambikizi ya COVID-19, ili kuwalinda wakimbizi ambao wako hatarini na jamii kwa ujumla. Kuna hitaji la haraka kuongeza maeneo ya kuwatenga watu na uwezo wa utoaji matibabu pamoja na kuongeza wigo wa upimaji kwenye maeneo mengi ya Kigoma. Makundi haya ya watu yaliyosahaulika, hata na ulimwengu, yanahitaji msaada wetu sasa kabla hatujachelewa.