MSF in Galkayo, Somalia
Access to Healthcare

Kusogeza huduma za matibabu kwa raia wanaoishi katikati mwa Somali

Galkayo, mji ulioko katikati mwa Somalia, unahifadhi idadi kubwa ya wakimbizi wa ndani ambao wamekimbia machafuko, ukame na madhara mengine ya mabadiliko ya tabia nchi yanayoikabili nchi hiyo. Mji huu pia una wahifadhi wahamiaji na wakimbizi pamoja na raia wengine kutoka mkoa wa Somali ulioko nchini Ethiopia wakitafuta huduma bora za afya.

Hospitali ya mkoa ya Mudug ndio hospitali pekee ya rufaa, ikihudumia watu karibu nusu milioni. MSF imekuwa ikisaidia hospitali hii tangu mwaka 2017. Leo hii, tunafanya kazi katika chumba cha dharura, tukiwahudumiwa watoto wanaosumbuliwa na utapia mlo, kutibu wagonjwa wa kifua kikuu, kusaidia wanawake wenye matatizo ya ujauzito na kutoa kliniki zinazohamishika. Hizi ni baadhi ya shuhuda za wagonjwa waliohudumiwa na MSF kwenye mji wa Galkayo.

“Mtoto wangu Farhiya alikuwa dhoofu sana na alikuwa haponi – alikuwa kama amezirai,” anasema Khadro Ahmed Abdi mwenye umri wa miaka 28. Wakati tulipofika hospitali kama saa 9 nilikuwa nimejawa na hofu. Wauguzi akwa haraka sana walimchukua na kumpeleka kwenye chumba cha dharura.”

Wakati mtoto wake wa kike mwenye umri wa miaka 11 alipougua, majirani wa Khadro walimshauri aende katika hospitali ya mkoa ya Mudug, ni muda wa saa 5 kutoka kwenye kijiji chao cha Jira’le, katika mkoa wa Somali nchini Ethiopia, akimuacha mtoto wake mwingine wa kike mwenye umri wa miaka 8 chini ya uangalizi wa mume wake. Famili hii ambayo kitamaduni ni ya wafugaji, inaishi katika eneo lenye ukame mkali na wanaishi kwa mlo mmoja tu kwa siku. Farhiya alikuwa na utapia mlo wa kiwango cha juu na muda aliofika Galkayo, alikuwa hajitambui. Wauguzi hawakutaka kupoteza muda kumuhudumia katika kitengo maalumu cha lishe cha hospitali hiyo.

“Baada ya kupokea huduma zote muhimu na maziwa yenye virutubisho pamoja na biskuti [Karanga, lishe na karanga zenye kalori], mtoto wangu alipata nafuu na siku mbili baadae tuliweza kurejea nyumbani,” anasema Khadro. Bila matibabu, anasema watoto wengi kama ilivyo kwa mtoto wake wa kike wasingeweza kupona.

msf287156_medium.jpg

Ukame na Mapigano

Takwimu za utapia mlo kwa watoto nchini Somalia ni suala lililozoeleka, hasa kwa familia ambazo hazina makazi kutokana na kukimbia mapigano na hali ya ukame na mara nyingi wamekuwa wakiishi katika maeneo masikini. Kati ya mwezi Januari na Agosti mwaka huu, MSF imetoa matibabu kwa watoto elfu 2 waliokuwa wanasumbuliwa na maradhi ya utapia mlo katika hospitali hii.

Uhaba mkubwa wa mvua katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni, ikisababisha umasikinina mazingira magumu ya kuishi, imechangia pakubwa kuongezeka kwa maradhi ya utapia mlo. Kwa mwaka huu nchi ya Somalia, inakadiriwa kuwa watoto laki 903,000 walio na umri wa chini ya miaka mitano wanakabiliwa na utapia mlo, wakiwemo laki 138,000 ambao wanasumbuliwa na hali mbaya ya utapia mlo, na hii ni kwa mujibu wa Unicef.

Bilal, mtoto wa miezi 8 amelala kando ya mama yake kitandani katika wodi ya watoto. Akiletwa hospitalini hapo na timu ya wataalamu wa MSF ambao wanatoa huduma za kutembea kutoka nyumbani kwake kwenye kambi ya Bulo Ba’ley inayohifadhi wakimbizi wa ndani, Bilal anaendelea akupata nafuu kutokana na kupoteza maji mengi kwa kuharisha.

“Bilal alikuwa akiharisha kwa siku tatu na alipoteza maji mengi,” anasema mama yake, Kawsar Ibrahim mwenye umri wa miaka 25, na ambaye mtoto wake wa miaka 3 yuko nyumbani na mume wake akifanya kazi za kawaida tu. “Alianza kupatiwa matibabu punde tu baada ya sisi kuwasili. Kwa sasa ameacha kuharisha na mtoto wangu anaendelea vizuri. Ninayo furaha sana kuwa mwanangu Bilal anaendelea vizuri na ataweza kwenda kucheza nyumbani tena.”

Siku tano baada ya kuletwa hospitali kwa matibabu, Bilal sasa yuko tayari kurejea nyumbani.

msf287167_medium.jpg

Hali mbaya ya maisha na kuwasili kwa watu wapya

Mji wa Galkayo umegawanyika mara mbili kwa mipaka ya kiutawala, huku kaskazini na kusini mwa kila upande kukiwa ni majimbo tofauti: Puntland na Galmudug. Idadi ya raia kwenye miji hii inaongezwa na watu wengine laki moja ambao ni wakimbizi wandani (IDPs) wakitoka maeneo mbalimbali ya Somalia, na wakiishi katika makambi wakiwa na rasilimali chache. Baadhi wamekuwa hawana makazi kwa miaka. MSF inasaidia hospitali hii kwa kutoa matibabu bure kwa watu waliokimbia makwao, wakimbizi na jamii zinazoishi kutoka katika miji yote miwili.

“Mji wa Galkayo kwa sasa una kambi zaidi ya 70 za wakimbizi wa ndani, huku watu wengi zaidi wakiendelea kuwasili kila wiki kutoka kwenye maeneo yenye machafuko na miko iliyokumbwa na ukame nchini Somalia,” anasema Bashir Muse Hassan, Meneja msaidizi wa MSF katika hospitali ya mkoa ya Mudug. “Timu ya matabibu wetu wanaotembea, wanatembelea kambi 23 karibu kila siku, wakitoa huduma za matibabu ya msingi na kuwahamishia katika hospitali wagonjwa wenye matatizo makubw aya kiafya. Wakimbizi wa ndani hawana maji ya kutosha au chakula kwa hivyo kuna idadi kubwa ya watoto wanaosumbuliwa na maradhi ya utapia mlo.

msf287152_medium.jpg

Changamoto wakati wa kujifungua

Sio watoto peke yao ndio wako hatarini kwenye mji wa Galkayo. Nchini Somalia idadi ya vifo vya mama na mtoto ni vya kiwango cha juu duniani. Kwa matabibu pamoja na familia za wanawake wajawazito, kudhibiti changamoto wakati wa ujauzito na wakati wa kujifungua ni mtihani mkubwa.

Deqa Awil Hassan, mwanamke mwenye umri wa miaka 32 na mama wa watoto 7, hivi karibuni alijifungua kwa upasuaji, kwa makubaliano na familia yake, baada ya madaktari kumtaarifu kuwa asingeweza kujifungua kwa njia ya kawaida.

“Nilikuwa katika wiki ya 25 ya ujauzito wangu wakati ukuta wa uzazi ulipoanza kutoa damu. Awali nilipelekwa katika hospitali ya Galdogob (mji wa Somali unaopakana ana Ethiopia) na kule madaktari walinielekeza katika hospitali hii,” anasema Deqa, ambaye anatoka kwenye wilaya zote, katika mkoa wa Somali nchini Ethiopia. “Huu ulikuwa ni ujauzito wangu wa 7 na nilikuwa nikiogopa kidogo. Kwa bahati nzuri nikajifungua mtoto mwenye afya wa kiume. Nashukuru kwa kuwa sote, mtoto wangu na mimi mwenyewe tuko salama. Nataka nimpe jina la ‘Abdi Nasib’ kwa sababu alikuwa na bahati ya kuzaliwa salama [jina hili lina maanisha mtumishi wa hatma].”

msf287161_medium.jpg

Mwezi Juni mwaka 2019, timu ya MSF katika hospitali ya mkoa ya Mudug, ilipokea wanawake zaidi ya 170 waliokuwa wanakabiliwa na matatizo ya ujauzito na zaidi 19 kati tao walikuwa wanahitaji upasuaji wa haraka. “Kutokana na idadi hii, unaweza kukadiria ni kwa kiwango gani huduma hii ni ya muhimu kwa jamii ya hapa,” anasema Bashir.

Uvujaji wa damu wa ndani kwenye ukuta wa uzazi ni jambo la kawaida wakati wa ujauzito, anaeleza daktari wa uzazi Abdullahi Mohamed Muse, na ni asilimia 30 ya wanawake wenye tatizo hili wanahitaji upasuaji. “Tunafuatilia na kutazama tatizo lenyewe kabla ya kuamia ikiwa tuingilie kati kuokoa maisha ya akina mama wajawazito na watoto wao walioko tumboni,” anasema Abdullahi. “Upasuaji huu [upasuaji wa dharura] unahitajika pale tu ambapo maisha ya mama yako hatarini. Tunajaribu kuwaeleza na kuzishawishi familia kuhusu umuhimu wa kuokoa maisha ya mama. Hii inaweza kusaidia kupunguza idadi ya vifo vya mama na mtoto nchini Somalia.

msf287169_medium.jpg

Kifua Kikuu

Timu ya MSF katika hospitali ya Mudug pia inafaya kazi ya kupunguza madhara ya ugonjwa kifua kikuu (TB), ugonjwa ambao unaambukizwa kwa urahisi katika eneo lenye msongamano wa watu, kama vile katika kambi zinazo wahifadhi wakimbizi wa ndani mjini Galkayo. Nchini Somalia, utambuzi na matibabu ya TB mara nyingi hayapatikani au unaweza kuwa sugu, jambo ambalo huenda likasababisha usugu wa dawa.

Kwa sasa kuna wagonjwa 172 ambao wote wameonesha dalili za usugu wa dawa na ambapo imekuwa ni sehemu ya mpango wa matibabu, mwanzoni mwa nusu mwaka wa 2019 karibu wagonjwa 100 walifanikiwa kumaliza matibabu yao. Licha ya mafanikio haya, bado kuna changamoto.a Nur Ahmed Nur, ambaye aliwahi kusimamia wodi ya wagonjwa wa TB tangu kuanzishwa kwake, anasema wagonjwa kutokamilisha matibabu kunaweza kuwa ni tatizo. Kusaidia kupunguza hili, timu yetu inafanya kazi na jamii na kuwahamasisha wagonjwa kwenda na ndugu zao ili wawasaidie wakati wa mchakato wa matibabu.

“Kuwafuatilia wagonjwa wote itatusaidia kuhakikisha wanapokea dawa kila siku,” anasema Nur. “Matokeo ya hatua hizi husaidia kuepusha mgonjwa kuwa sugu wa dawa za TB.”

Fardowsa Hussein Hassan mwenye umri wa miaka 40, kutoka kaskazini mwa mji wa Galkayo, alipata TB ya mfumo wa upumuaji. Alimaliza kikamilifu matibabu yake mwezi Juni, lakini amekuwa akirejea hospitalini kwa uchunguzi wa mara kwa mara.

“Nilikuwa dhaifu na mgonjwa sana wakati nilipoletwa hospitali mwezi Januari,” anasema Fardowsa. “Nilikuwa nikikohoa kwa majuma kadhaa na wakati madaktari walipochukua makohozi yangu kuyapeleka maabara, niligundulika kuwa na TB. Haraka sana nilianza kutumia dawa. Miezi sita baadae nimepima na sina tena TB. Naushukuru uongozi wa hospitali na wale wote wanaokisaidia kitengo cha TB.”


MSF imefanya kazi Somalia na Somaliland tangu mwaka 1991. Mwaka 2013, ililazimika kusitisha huduma zake baada ya mfululizo wa mashambulizi dhidi ya wafanyakazi wake. Wataalamu wetu walianza kutoa tena huduma miaka minne baadae, mwezi Mei mwaka 2017, kutokana na uhitaji mkubwa wa changamoto za afya ambazo zilikuwa zikihitajika na wananchi. MSF inatoa matibabu ya awali na kwa wagonjwa wa ndani katika hospitali, kliniki zinazotembea zikiwalenga watu ambao mara zote wamekuwa wakihamahama kama vile wakimbizi, wakimbizi wa ndani na wahamiaji, na sasa MSF inafanya kazi Somaliland kwenye mii ya (Hergeisa, Borama, Berbera, Las Anod), Puntland (Galkayo Kaskazini) na kusini magharibi mwa Baidoa. MSF inahamasisha shughuli za kuingia na kutoka kwenye mji wa Jubaland, ikijikita katika huduma za lishe na huduma za dharura. Katika majuma kadhaa yajayo, MSF itaanza kutekeleza shughuli za huduma za kuokoa maisha katika sehemu za vitengo vyake kule Kusini mwa hospitali ya Galkayo kwenye jimbo Galmudug.

msf288088_medium_0.jpg